Ujumbe wa Jaden Smith kwa Jackie Chan

Baada ya miaka 16 kupita tangu walipokutana kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya The Karate Kid, nyota wa filamu na mwanamuziki Jaden Smith ametoa ujumbe kwa Jackie Chan akimshukuru kwa mchango wake wa kukitambulisha kipaji chake katika tasnia ya burudani
Jaden ameshare ujumbe huo katika ukurasa wake wa instagram akimtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa ambapo alieleza namna Chan alivyobadilisha maisha yake.
“Nakupenda, umebadilisha maisha yangu na umenifundisha mambo ambayo sitasahau kamwe. Siwezi kuwa nilivyo leo bila wewe. Wewe ni gwiji, kielelezo na kiongozi. Heri ya siku ya kuzaliwa, tutaonana hivi karibuni.”

Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2010 kupitia filamu ya The Karate Kid, ambapo Jackie Chan alicheza nafasi ya mwalimu na Jaden Smith akiwa mwanafunzi wake wa karate. Filamu hiyo ilipata mafanikio makubwa na kumtambulisha Jaden katika anga la kimataifa la uigizaji.
Tangu wakati huo, uhusiano wao umeendelea kuwa wa heshima na kumbukumbu, ukiwakutanisha tena kwa namna ya kipekee baada ya miaka 16, huku mashabiki wakieleza furaha yao kuona urafiki huo wa kisanaa ukidumu kwa muda mrefu.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.