Marioo Aweka Dau la Milioni 2 kwa Dance Challenge ya Wimbo Wake “Sugar”
Marioo Atoa Sh2 Milioni kwa Dance Challenge ya Wimbo Wake Mpya “Sugar”
Mwanamuziki wa Bongo Flava Marioo ameibua gumzo kubwa baada ya kutangaza dau la Sh2 milioni kwa dancer atakayefanya dance challenge bora ya wimbo wake mpya “Sugar”.
Kupitia tangazo lake, Marioo aliwahamasisha dancers na mashabiki kuonesha vipaji vyao kupitia challenge hiyo, akisisitiza ubunifu na uwezo wa kipekee.
“Kama wewe ni dancer mkali, tuoneshe uwezo wako! Kuna dau la Sh2 milioni kwa atakayefanya dance challenge kali ya Sugar,” alisema Marioo.
Vigezo vya Kushiriki Challenge ya Marioo “Sugar”
- Ubunifu wa dance uwe wa kipekee
- Energy na performance iwe ya juu
- Video iwe na mvuto na ubora mzuri
- Challenge iwe tofauti na nyingine
Marioo aliongeza kuwa mshindi atachaguliwa kulingana na ubora wa dance na namna itakavyovutia mashabiki mtandaoni.
Wimbo wa “Sugar” umetayarishwa na producer maarufu S2kizzy kutoka studio za Pluto Republic, huku video yake ikiongozwa na Director Fole X, jambo linaloongeza ubora wa kazi hiyo mpya.
Challenge hii inatarajiwa kuibua vipaji vipya vya dancers na kuongeza umaarufu wa wimbo huo katika mitandao ya kijamii kama TikTok, Instagram na YouTube.


No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.