King Kiba na Mbosso kwenye dude moja

Kuna dude linapikwa. Limepikwa. Litapikwa. Sijui lipo hatua gani au linatolewa leo. Kifupi ni 'kolabo' ya King Kiba na Mbosso Khan. Hii ni vita nyingine isiyoumiza na zaidi ni yenye kufurahisha, hawa ni mafundi wawili wa nyakati za leo na jana.
Tumkumbushe Mbosso Khan, kwamba kwa King Kiba siyo Bien pekee. Kuna balaa alikutana nalo Baraka Da Prince akiwa wa moto. Kuna Rayvanny, Barnaba, Whozu, Jay Melody na kaka yao Ommy Dimpoz hata marapa wakubwa.
King Kiba sauti ndo silaha yake kubwa. Lakini pia ana mashabiki watiifu sana ambao wana uwezo wa kulazimisha nyekundu ikawa njano. Na ukijichanganya kwenye video katika 'ishu' ya muonekano atakumaliza jumla na kukuzika.
Lakini pia King Kiba tunampa tu angalizo. Kwamba 'bwa' mdogo' Mbosso Khan, ukimfunika kwa sauti atakuja na utunzi. Ukimuua na utunzi, atakuumiza na melodi, unatakiwa uwe makini kwa kila kitu na usichukulie poa ukajikuta unajutia.
Baada ya kutoka WCB, konde Boy amekuwa akiwsfunika wenzake kwenye 'kolabo'. Kuanzia Marioo mpaka Rayvanny na wengine wa kutosha. Jzi kati kaingiza anga za Mbosso Khan, kachapika na kasuuzwa vibaya sana na dunia inajua.
Sasa tunapowakumbusha wote, Alikiba atambue anashirikiana na fundi. Na Mbosso atambue yule anayeshirikiana naye ni Ally Kiba. Wasifanye kazi kimazoea mmoja akajutia ujio wa 'projekti' yao hii kwa kujitakia.
Kimsingi. Hii siyo vita, lakini hili ni tatizo lingine linakwenda kutokea mjini. Huu ni msala mpyas mjini. Ni mtiti unaokuja kuzima redio mbao. Hili ni bonge la 'kolabo' la kutoks kwa mafundi watupu na wssio ns makeke. Hulka na tabia zao zinafanana.

👉 Soma zaidi: Nyimbo Mpya Tanzania
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.