-->

Breaking News

Fahamu haya kuhusu Nikki wa Pili

 Fahamu haya kuhusu Nikki wa Pili

Msanii wa Hip Hop Bongo, Nikki wa Pili ni miongoni mwa wasanii watano wanaounda kundi la Weusi, huku akiwa amefanya muziki kwa zaidi ya miaka 10 na kujizolea mashabiki wengi.

Nikki wa Pili ambaye kwa sasa ni mkuu wa Wilaya ya Kibaha, ametoa nyimbo nyingi ambazo zimefanya vizuri na kulitangaza vizuri jina lake. Fahamu zaidi.

1. Nikki wa Pili alikuwa anajua ana uwezo wa muziki, lakini hakujiona akifanya muziki kwa ukubwa, ni hadi pale kaka yake, Joh Makini, alipomwambia waongozane hadi studio akaone kazi zinavyofanyika. Wakati huo Nikki alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), basi walifika studio kwa G Solo (Kama Kawa Records) ambapo tunaweza kusema ndipo safari yake ilianza rasmi.

2. Pale studio akapewa mdundo na kuchana vizuri tu. Basi akaambiwa achane vesi nyingine na ndio iliyokuja kuwekwa katika wimbo alioshirikishwa na Joh Makini, Niaje Ni Vipi (2010) chini ya Kama Kawa.

3. Hadi sasa Joh Makini na Nikki wa Pili wameshafanya nyimbo nyingi pamoja na kwenye kundi la Weusi, lakini kuna wimbo mmoja ambao Nikki hawezi kuusahau katika nyimbo zaidi ya 10 walizoshirikiana. Wimbo huo ni Niaje Ni Vipi kwa sababu ndio kolabo yao ya kwanza na ndio uliomtambulisha vizuri kwenye muziki wa Bongofleva na kumpatia mashabiki wengi.

4. Nikki wa Pili ndiye aliyefanya Prodyuza Mona Gangster kuipa studio yake jina la Classsic Sound. Ni baada ya kutaja jina hilo mwanzoni mwa wimbo wake, Kiujamaa (2011) ambao Mona na Nahreel wamehusika kuutengeneza. 

5. Mdundo wa wimbo wa Nikki wa Pili, Good Boy (2010), alipou sikia tu alimpatia G Solo Sh60,000 ili akaurekodi. Basi akafanya vesi zake tatu kisha akamtafuta Rama Dee ambaye ameimba kiitikio cha wimbo huo.

6. Nikki wa Pili ndiye msanii wa kwanza kuwashirikisha Navy Kenzo kwenye wimbo wake. Alifanya hivyo katika wimbo, Safari (2015) ambao ulishirikisha wasanii wengine kama Joh Makini, G Nako, Jux na Vanessa Mdee.

7. Kipindi anaanza muziki, Dayna Nyange alikuwa akifanya rap na sio kuimba kama ilivyo sasa. Nikki wa Pili ndiye alimshauri kuachana na rap kwa sababu wasanii wa kike kwenye rap ni vigumu kutoka na kufanya vizuri. Dayna aliyetamba na ngoma zake kama Mafungu (2009) na Nivute Kwao (2011), siyo msanii pekee wa kike kutoka kwenye rap hadi kuimba hapa Bongo, kuna Vanessa Mdee, Lady Jaydee na Aika wa kundi la Navy Kenzo.

8. Wakati Whozu akijitafuta kimuziki, na akiwa mwanafunzi wa Chuo cha Ushirika Moshi, Nikki wa Pili ndiye alikuwa anamshauri sana njia za kupita ili kufanikiwa kimuziki, na hata alimchagulia wasanii kuwasikiliza ili kujifunza.

9. Nikki wa Pili, Joh Makini na Bonta walitokea kundi la River Camp kisha wakajiunga na wenzao wa Nako 2 Nako ambao ni G Nako na Lord Eyes, kisha likazaliwa kundi la Weusi ambalo lina albamu moja, Air Weusi (2021).

10. Vilevile Nikki wa Pili alikuwa miongoni mwa wasanii watatu walioshiriki katika wimbo wa kwanza uliowapatia Weusi mafanikio, Gere (2013) ambao uliwafanya kushinda tuzo mbili za muziki Tanzania (TMA) 2014

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.