Celine Dion kurudi jukwaani, baada ya miaka minne

Mwanamuziki Celine Dion, ametangaza rasmi kurejea jukwaani ikiwa ni miaka minne tangu alipogundulika kuwa na ugonjwa adimu usiotibika uliokuwa umeathiri sauti yake na uwezo wa kutembea.
Nyota huyo anayejulikana kupitia nyimbo maarufu kama My Heart Will Go On na Because You Loved Me, anatarajiwa kufanya ‘shoo’ 10 katika ukumbi wa Paris La Défense Arena, mbele ya mashabiki wapatao 40,000 kuanzia Septemba hadi Oktoba mwaka huu.
Tangazo hilo limekuja wakati Dion akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 58, ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kurejea kwake kama zawadi bora zaidi ya maisha yake.
“Niko tayari kufanya hivo, Najisikia vizuri, nina nguvu, nina msisimko, niko wazi na, bila shaka, nina wasiwasi kidogo,” amesema.
Akizungumzia hali yake ya kiafya, mwanamuziki huyo amesema anaendelea vizuri huku akisimamia afya yake kwa karibu.

Ikumbukwe Celine anaugua ugonjwa adimu wa mfumo wa neva unaojulikana kama Stiff Person Syndrome (SPS) ambao husababisha misuli kukakamaa na kuathiri sauti pamoja na uwezo wa kutembea. Ugonjwa huu ulianza kumsumbua tangu 2008 na kumfanya asimamishe shughuli za muziki kwa miaka minne tangu 2022.
Celine alifichua katika mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari kuwa dalili za ugonjwa zilianza muda mrefu lakini madaktari walingundua ugonjwa huo Desemba 2022.
SPS ni ugonjwa usiotibika kabisa, lakini tiba zinazotolewa husaidia kudhibiti dalili ili kumwezesha mgonjwa kuishi na kufanya shughuli zake. Ugonjwa huo unampata mtu 1 kati ya milioni moja.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.