-->

Breaking News

Winnie staa mwenye vitiligo anayetikisa duniani

 Winnie staa mwenye vitiligo anayetikisa duniani

Kadri tasnia ya urembo inavyozidi kukua watu wenye ugonjwa wa ngozi ufahamikao kama ‘Vitiligo’ wanazidi kung’ara na kuonyesha kuwa tofauti si kasoro bali ni zawadi toka kwa Mungu.

Chantelle Young Brown maarufu kama Winnie Harlow ni moja ya wanamitindo wakubwa duniani mwenye ugonjwa wa Vitilio aliyebadili mitazamo ya jamii kuhusiana na ugonjwa huo

Winnie alizaliwa Julai 27, 1994, nchini Kanada. Akiwa na umri wa miaka minne, aligundulika kuwa na ugonjwa wa ngozi ‘Vitiligo’, hali inayosababisha kupotea kwa rangi ya ngozi katika baadhi ya maeneo ya mwili. Tangu akiwa mdogo, hali hiyo ilimtofautisha na wenzake tofauti ambayo haikukubaliwa kirahisi.

Akiwa shuleni, alikumbana na unyanyapaa mkali. Aliitwa majina kama “punda milia” na “ng’ombe”, kejeli zilizomuumiza kisaikolojia na hata kumfanya abadilishe shule mara kadhaa. Wakati mwingine alifikia hatua ya kutaka kukata tamaa kabisa. Lakini ndani yake kulikuwa na nguvu ambayo sasa imebadilisha maisha yake.



Mungu si Athumani kupitia mitandao ya kijamii mtangazaji maarufu Tyra Banks, alikumbana na Winnie akampata nafasi ya kushiriki katika kipindi maarufu cha America’s Next Top Model mwaka 2014.

Ingawa hakushinda shindano hilo, alijijengea jina na kuonekana tofauti kabisa na washiriki wengine. Muonekano wake wa kipekee uliwavutia wabunifu na wapiga picha wa mitindo.

Baada ya kipindi hicho, milango ilianza kufunguka. Winnie alichaguliwa kuwa model wa kampeni ya chapa ya Desigual, na pia akaonekana katika matangazo ya kampuni ya Diesel. Kuanzia hapo, alitembea kwenye majukwaa makubwa ya mitindo, akafanya kazi na wabunifu wakubwa, na kuonekana kwenye majarida maarufu duniani ikiwemo hili la Starehe.

Amekuwa akipaza sauti kila siku kwa watu wenye vitiligo, akihamasisha kujikubali.”
“Nilijipenda, na hapo ndipo fursa zilipoanza kunifuata,” Moja ya maneno yake.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.