Mitandao ya kijamii yabadili maisha ya wazazi wa mtoto Krish Mondal

Mitandao ya kijamii inaendelea kuthibitisha kuwa ni jukwaa lenye nguvu kubwa ya kubadilisha maisha ya watu duniani, likiwezesha vipaji vilivyokuwa vimefichika kujitokeza na kutambulika katika pande zote za dunia.

Hali hiyo imejidhihirisha kupitia mtoto Krish Mondal mwenye umri wa miaka 9, ambaye kupitia kipaji chake cha kuimba amefanikiwa kubadilisha maisha ya familia yake.
Krish, akiwa pamoja na kaka yake Kishore Mondal, walianza kutengeneza maudhui ya kuimba kwa lengo la kujifurahisha. Lakini miezi michache baadaye maudhui hayo yalianza kuwapa matumaini ya kutoboa kimaisha, baada ya kurekodi video fupi wakiimba wimbo “Jeene Laga Hoon” wa Atif Aslam, hatua iliyowafungulia milango na kufahamika zaidi.
Video hiyo ilisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali na kuwafikia watazamaji wengi duniani, ambao waliwapongeza kwa uwezo wao wa uimbaji na sauti zao zilizogusa hisia za wengi. Umaarufu wao uliendelea kukua na kufikisha zaidi ya wafuasi milioni 4.5 katika ukurasa wao wa Instagram.

Kwa kuongezeka kwa umaarufu huo, maisha ya familia yao yalianza kubadilika taratibu, huku wakipata fursa za kufanya matangazo, kutumbuiza katika majukwaa makubwa lakini pia kufanya kolabo na wasanii wengine.
Inaelezwa kuwa maisha yao yalibadilika kwa kiasi kikubwa kwani wamefanikiwa kununua nyumba mpya, kuishi maisha yenye hadhi kidogo lakini pia kumuhamisha Krish kwenye shule bora.
Krish Mondal alizaliwa Novemba 20, 2017 huko Howrah katika jimbo la West Bengal, India. Amekua akifanya vizuri katika mitandao ya YouTube akikusanya Zaidi wafuatiliaji 2.65 milioni pamoja na watazamaji Zaidi ya milioni 15 katika baadhi ya video zake.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.