-->

Breaking News

Universal Music Group East Africa kufanya kazi na Lady Jaydee

 Universal Music Group East Africa kufanya kazi na Lady Jaydee

Kampuni ya kusaini na kusimamia wasanii Universal Music Group East Africa imetangaza kufanya ushirikiano na mkongwe wa Bongo Fleva Lady Jaydee ambaye anatambulika kama mmoja wa msanii mwenye ushawishi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ushirikiano huo ni hatua ambayo inaelezwa kuwa ni mkakati kwa Universal Music Group East Africa kuibua, kukuza na kusambaza sauti bora zaidi kutoka Afrika Mashariki hadi kwenye majukwaa ya dunia.



Kupitia ushirikiano huu, pande zote mbili zimejipanga kuinua kiwango cha ubunifu wa muziki wa Afrika Mashariki, kupanua wigo wake wa usikivu duniani, na kuimarisha nafasi yake katika jukwaa la kimataifa.

Universal Music Group East Africa imeeleza furaha yake kufanya kazi na wasanii wenye maono, uzoefu na dhamira ya ubora. Imebainisha kuwa uwepo wa Lady Jaydee katika ushirikiano huo unaonesha heshima kwa historia yake ya muziki, huku ukitoa msukumo mpya wa kusonga mbele. Pia imeeleza matarajio ya kujenga juu ya msingi aliouweka na kufikia mafanikio makubwa kupitia malengo ya pamoja.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.