Siri Shah Rukh Khan kuendelea kung’ara Bollywood

Mwigizaji wa Bollywood Suniel Shetty amefichua sababu zinazofanya Shah Rukh Khan kuendelea kuwa maarufu huku ikiwa ni ngumu umaarufu wake kufiukiwa na waigizaji wengine.
Akizungumza katika podikasti ya Raj Shamani, Shetty alisema mafanikio makubwa ya Shah Rukh Khan hayajaja kwa bahati mbaya bali ni mchanganyiko wa kipaji, bidii pamoja na uwezo wa kubadilika kulingana na muda unavyosonga.

Kwa mujibu wa Shetty, moja ya sababu kubwa iliyomsaidia Shah Rukh kufika mbali ni muziki uliokuwa ukiambatana na filamu zake. Alieleza kuwa katika tasnia ya filamu nchini India muziki una nafasi kubwa sana, na nyota huyo aliweza kupata nyimbo zilizogusa hisia za mashabiki wengi.
Pia alimpongeza kwa kufanya kazi kwa karibu na mtayarishaji maarufu wa filamu Yash Chopra, ambaye alichangia kutengeneza baadhi ya filamu na nyimbo zilizokuwa maarufu sana.
Shetty aliongeza kuwa Khan amekuwa akijituma sana katika kazi yake na kila wakati hujaribu kujibadilisha ili kuendana na mabadiliko ya tasnia ya filamu. Alisema haiba yake, nidhamu ya kazi pamoja na heshima anayotoa kwa watu wanaomzunguka ndiyo mambo yanayomfanya aendelee kupendwa na mashabiki duniani kote.
Mwigizaji huyo pia aligusia suala la mitandao ya kijamii akisema Khan si miongoni mwa mastaa wanaotegemea sana majukwaa hayo kupata umaarufu, badala yake anatumia mbinu za mastaa wazamani ambao walijijenga kupitia kazi zao na sio kelele za mitandaoni.
Katika maelezo yake, Shetty alimlinganisha nyota huyo na mwigizaji Ranbir Kapoor, ambaye hana akaunti rasmi za mitandaoni na mara nyingi hufuatilia tu taarifa kupitia akaunti binafsi ya siri, akiamini kuwa kazi yake ndiyo inayopaswa kuzungumza kwa niaba yake.
Kwa upande mwingine, Shah Rukh Khan hutumia mitandao ya kijamii mara chache, hasa kutangaza kazi zake mpya. Hata hivyo, licha ya uwepo huo mdogo, bado anatajwa kuwa mmoja wa mastaa wakubwa zaidi katika historia ya Bollywood.
Nyota huyo alianza safari yake ya uigizaji kupitia vipindi vya televisheni kabla ya kuingia kwenye filamu na kujipatia umaarufu kwa kuigiza nafasi za uhalifu katika filamu kama Baazigar na Darr. Baadaye alijijengea jina kama mfalme wa filamu za mapenzi kupitia kazi kama Dilwale Dulhania Le Jayenge, Kuch Kuch Hota Hai, Kabhi Khushi Kabhie Gham, Devdas na Veer-Zaara.

Kwa miaka mingi pia ameendelea kutoa filamu zinazofanya vizuri kibiashara na kumuingizia mkwanja mrefu kama Om Shanti Om, Chak De! India, Don 2 na Chennai Express.
Aidha mwaka 2018 alikumbana na changamoto ya mapato ya filamu jambo ambalo lilisababisha kupumzika kwa takribani miaka 4 ambapo mwaka 2023 alirudi kwa kishindo akiachia filamu tatu zilizofanya vizuri Kimataifa ikiwemo Pathaan, Jawan na Dunki. Kupitia filamu ya Jawan, alishinda tuzo ya National Film Award for Best Actor mwaka 2025.
Kwa sasa Khan anatarajia kuachia filamu yake iitwayo King, inayoongozwa na Siddharth Anand huku ikiwashirikisha mastaa kama Deepika Padukone, Suhana Khan, Abhishek Bachchan na Jaideep Ahlawat, ikitarajiwa kuanza kuonyeshwa katika kumbi za sinema Desemba 25, 2026.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.