-->

Breaking News

Siri kuishi maisha marefu ni kukaa mbali na wanaume

 Siri kuishi maisha marefu ni kukaa mbali na wanaume

Mwanamke mkongwe kutoka Scotland, Jessie Gallan alifichua siri ya kuishi maisha marefu na yenye afya, akieleza kuwa miongoni mwa mambo aliyoyazingatia ni kula lishe bora, kufanya mazoezi mara kwa mara na kuepuka wanaume.

Wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya Uingereza enzi za uhai wake, Gallan alisema katika maisha yake yote hakuwahi kuolewa, huku akiamini kuwa kukaa mbali na wanaume kumemsaidia kuepuka matatizo mengi.

“Siri yangu ya kuishi maisha marefu ni kukaa mbali na wanaume kadri inavyowezekana. Unapata matatizo mengi kuliko faida kutoka kwao,” alisema Gallan.



Mbali na hilo, alisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi na lishe bora, akibainisha kuwa amekuwa akihakikisha anafanya mazoezi kadri awezavyo na kula uji wa moto kila siku.

“Nimekuwa nikihakikisha nafanya mazoezi mara kwa mara, nakunywa uji mzuri wa moto na sijawahi kuolewa,” aliongeza.

Aidha kikongwe huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa Januari 2,2015 ambapo alitimiza miaka 109, lakini alifariki mwezi mmoja baadaye akiwa nyumbani kwake Aberdeen, Scotland.

Hata hivyo, utafiti wa kitaifa wa watu waliofikisha umri wa zaidi ya miaka 100 nchini Marekani uliofanyika mwaka uliopita, umeonyesha kuwa mbali na lishe na mazoezi, kutumia muda mwingi na familia pamoja na marafiki pia ni miongoni mwa siri muhimu za kuishi maisha marefu.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.