Oscar 2026 ilivyonoga, Michael B. Jordan anyakua kwa mara ya kwanza

Tuzo za 98 za Academy Awards maarufu kama Oscar zimefanyika usiku wa Machi 15, 2026 katika ukumbi wa Dolby Theatre jijini Los Angeles, Marekani, zikikusanya mastaa wakubwa wa filamu duniani.
Katika sherehe ya tuzo hizo iliyoendeshwa na mchekeshaji maarufu Conan O'Brien. Ilihudhuriwa na waigizaji, watayarishaji, wabunifu wa mitindo na wapenzi wa filamu kutoka sehemu mbalimbali dunia. Huku zulia jekundu likiwa kivutio kikubwa kutokana na mavazi ya kifahari waliovaa mastaa.
Kwa mwaka huu 2026 ushindi mkuu wa tuzo hizo ulienda kwenye filamu ya One Battle After Another ikitwaa tuzo ya Filamu Bora (Best Picture) pamoja na tuzo nyingine kadhaa, na hivyo kuwa mshindi mkuu wa Oscar 2026.
Miongoni mwa washindi wengine ni Muongozaji Bora Paul Thomas Anderson, Mwigizaji Bora wa Kiume Michael B. Jordan kupitia filamu ya Sinners. Mwigizaji Bora wa Kike Jessie Buckley kupitia filamu ya Hamnet.
Wengine ni Mwigizaji Msaidizi Bora wa Kiume Sean Penn na Mwigizaji Msaidizi Bora wa Kike ni Amy Madigan. Hatahivyo filamu ya 'Sinners' ilifanya vizuri kwa kushinda tuzo kadhaa ikiwemo Screenplay Bora ya Asili, Muziki Bora na Sinematografia.
Mbali na hayo filamu nyingine zilizoshinda Filamu Bora ya Kimataifa ni Sentimental Value, filamu ya Norway. Filamu Bora ya Uhuishaji, KPop Demon Hunters. Wimbo Bora Golden kutoka KPop Demon Hunters, Filamu Bora ya Nyaraka Mr. Nobody Against Putin, Filamu Bora ya Visual Effects Avatar: Fire and Ash na yenye Sauti Bora F1.
Mambo mengine yaliyovutia katika tuzo hizo ni filamu ya One Battle After Another iliongoza kwa idadi ya tuzo sita. Sinners ndiyo ilikuwa katika uteuzi nyingi ikiteuliwa mara (16).
Pia hii inakuwa mara ya kwanza kwa Michael B. Jordan kushinda Oscar. Jambo jingine la kuvutia ni Jessie Buckley kuweka historia kama Muirish wa kwanza kushinda tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.