-->

Breaking News

Kumbe Airpods zinavaliwa hivi

 Kumbe Airpods zinavaliwa hivi

Kumbe Airpods zinavaliwa hivi

Imebainika kuwa watumiaji wengi wa vifaa vya masikioni aina ya AirPods Pro kutoka kampuni ya Apple Inc, wamekuwa wakivaa vifaa hivyo kwa njia isiyo sahihi jambo ambalo linasababisha visikae vizuri au kutoa sauti isiyoridhisha.

Kwa mujibu wa mwongozo rasmi wa matumizi ya AirPods Pro inaelezwa kuwa mtumiaji anatakiwa kuvaa kifaa hicho kama ambavyo inaonekana kwenye picha. Hatua hiyo inasaidia kutengeneza mfuniko mzuri wa sauti (acoustic seal), unaoboresha ubora wa bass pamoja na uwezo wa kuzuia kelele kutoka nje.



Hata hivyo, watu wengi wamekuwa wakikiingiza kifaa hicho moja kwa moja bila kukizungusha, jambo linalosababisha kisionekane kuwa na ubora wake kamili na hata kudondoka kirahisi wakati wa harakati kama mazoezi au usafiri.

Aidha taarifa hiyo imezua mjadala katika mitandao ya kijamii. Ambapo watumiaji mbalimbali wameonesha kuvutiwa na uvaaji sahihi wa kifaa hicho huku wakieleza tangu waanze kutumia njia hiyo wamekuwa wakisikiliza muziki bila usumbufu wowote.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.