-->

Breaking News

Orodha ya wachezaji wa Yanga SC watakaokosekana mchezo vs TRA United


TRA United vs Yanga SC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba huku mabingwa watetezi wakiwakosa nyota wanne kuelekea mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti.

Taarifa rasmi kutoka Yanga SC imeeleza kuwa wachezaji hao watakuwa nje kwa mujibu wa ripoti ya madaktari na mchezo ambao wote wataukosa ni ule unaofuata dhidi ya TRA United.

Ibrahim Abdullah (Bacca) amepata jeraha la nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha Wiki tatu

Laurindo Dilson (Depu) amepata majeraha ya nyama za paja na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

Chadrack Boka amepata jeraha la enka ya mguu wa kushoto na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

Edmund John amepata jeraha la Bega na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

Mbali na wachezaji hawa wanne ikumbukwe kwamba Clement Mzize na Dickson Job nao hawatakuwa kwenye mpango wa mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.