-->

Breaking News

Mkoba huu kutoka Balenciaga unauzwa Sh 4.4 milioni

 Mkoba huu kutoka Balenciaga unauzwa Sh 4.4 milioni

Mwigizaji wa China, Zhang Jingyi, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuonekana hadharani akiwa amebeba mkoba wa kifahari kutoka Balenciaga lililopewa jina la ‘Trash Bags Large Pouch’

Kinachozua mijadala Zaidi si kwa mwonekano wa mwigizaji huyo bali ni kwa mwonekano wa mkoba huo ambao unafanana kabisa na mfuko wa kawaida wa kuwekea taka ambao unaopatikana majumbani.

Kupitia mitandao ya kijamii, watumiaji wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kwa kejeli na utani, wakisema kuwa muundo kama huo hauhitaji gharama kubwa kwani tayari upo katika matumizi ya kila siku kwa bei nafuu au hata bure.

‘Trash Bags Large Pouch’ inauzwa kwa gharama ya dola 1,790 ikiwa ni Zaidi ya Sh 4.4 milioni.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.