-->

Breaking News

Akon: Afrika ni salama kwa malezi ya watoto

 Akon: Afrika ni salama kwa malezi ya watoto

Mwanamuziki na mwigizaji kutoka Marekani, Aliaune Damala maarufu Akon ameweka wazi kuwa Afrika ndio nchi salama kwa malezi ya watoto kutokana na mfumo wa maisha na nidhamu iliyojijengea.

Ikumbukwe Akon alizaliwa na kukulia nchini Senegal kabla ya wazazi wake kuhamia Marekani akiwa na miaka saba.

Akon alizungumza hayo baada ya kuona baadhi ya tabia za mwanae Mohammed Thiam, ambazo haridhishwi nazo, hali iliyomfanya kulinganisha malezi ya watoto kati ya Afrika na Marekani.

Aliongeza kuwa uhuru nchini Marekani ni mkubwa kupita kiasi na kuwafanya vijana wadogo kuingia kwenye mambo ambayo hayana manufaa kwa maisha yao ya baadae.

"Unapokuwa bize kutafuta maisha na kufanya kazi kwa bidii, kama ilivyo kwa watu wengi barani Afrika, mara nyingi unakuwa huna muda wa kujihusisha sana na mambo yasiyo ya msingi kama kupoteza muda kwenye mitindo ya mavazi au kujipodoa kupita kiasi ila kwa Marekani ni tofauti,"€ alisema Akon.

Mkali huyo wa kibao cha 'Blame It on Me' alisisitiza kuwa wazazi wa Kiafrika wana nafasi kubwa ya kutengeneza vijana wenye nidhamu ya hali ya juu ambayo huwasaidia kukua kwenye misingi imara.

"Kuna muda jicho tu la mzazi mtoto anajirekebisha hapo hapo kabla hata hajapewa adhabu kubwa, malezi yenye msimamo na nidhamu ni muhimu kwa watoto na huwasaidia katika maadili."


Nyota huyo anawatoto tisa kutoka kwa wanawake tofauti, mke wake Tomeka Thiam, amepata naye watoto watano ambaye ni Alioune Thiam, Alianna Thiam, Jhavor Thiam, Journey Thiam na Muhammad Thiam. Huku majina ya watoto wengine yakiwa hayajaweka wazi.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.