-->

Breaking News

Binti wa Michael Jackson adai mgao wa mali

 Binti wa Michael Jackson adai mgao wa mali

Baada ya wiki iliyopita kuzuka taarifa watu wanne ndugu wa familia moja wamefungua kesi ya kudai mali dhidi ya marehemu Mfalme wa Pop, Michael Jackson, kuna kesi nyingine imefunguliwa na binti wa mwanamuziki huyo, Paris Jackson.

Inaelezwa Paris anaendelea kupambana kisheria na wasimamizi wa mali za baba yake, Michael Jackson kesi ambayo imekuwa na mgogoro wa muda mrefu unaoendelea mahakamani Marekani.

Kutokana na kesi iliyowasilishwa Februari 26, Paris amewashtaki wasimamizi wa mali za baba yake kufanya kesi hiyo kuwa ya gharama kubwa na kutumia muda mrefu zaidi.

Mgogoro ulizuka baada ya wasimamizi wa mali za Michael Jackson kuwasilisha ombi la kuondoa kesi ambazo zinadaiwa kuzuia au kuadhibu mtu kwa kutumia haki yake ya kuzungumza au kushiriki masuala ya umma.

Hatua hiyo ilikuja kama majibu ya ombi la Paris alilotaka mahakama ibadilishe utaratibu wa jinsi wasimamizi wa mali hiyo wanavyodai ada za mawakili kutoka kwenye mali ya marehemu.

Mahakama ilikubali ombi la kuondoa kesi, lakini mawakili wa Paris wanadai uamuzi huo haukubadilisha chochote katika madai yake ya msingi.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, walieleza ombi hilo halikufuta madai yoyote ya Paris na kilichofanyika ni kuchelewesha mchakato wa kesi.

Januari mwaka huu wasimamizi wa MJ waliwasilisha ombi jingine mahakamani wakitaka walipwe zaidi ya Dola 115,000 za Marekani kama gharama za mawakili zilizotumika kushughulikia ombi hilo. Kiasi hicho kinajumuisha takribani Dola 93,924 za ada za mawakili pamoja na gharama nyingine.

Lakini upande wa mawakili walitoa pingamizi suala la kiasi hicho kwamba kingeweza kupunguzwa gharama kwa kuwasilisha nyaraka kwa namna tofauti bila kuongeza gharama kubwa.

Wakati mgogoro huo ukiendelea kushika kasi nyaraka za awali zilizowasilishwa mwaka 2025 zinaonyesha kuwa Paris tayari alipokea kiasi cha Dola 65 milioni kwenye mali za baba yake ingawa mtoto mwenyewe alikataa kuwa hakupokea kiwango hicho cha fedha.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.