Komedi inavyompaisha Anko Nzala

Olipa Assa
Kuna maisha flani huja yenyewe hapa duniani kutokana na kazi au kipaji ulichojaliwa na Mwenyezi Mungu. Na hivi ndivyo ilivyo kwa Aman Nzalla maarufu kama Anko Nzalla.
Katika mahojiano na Mwananchi na mchekeshaji huyo maarufu hapa nchini, Nzalla anasimulia namna safari yake ilivyokuwa ngumu hadi kufikia hatua ya kipaji chake kujulikana.
Anasema kuna wakati alilazimika kushinda njaa akiamini ipo siku uvumilivu utamlipa na wakati huohuo hawakukosekana watu waliojaribu kumkatisha tamaa, lakini kwake hiyo ilikuwa ni fursa ya kujipanga atafanya kitu gani kipya kitakachofanya kipaji chake kifanikiwe.
"Baada ya kumaliza kidato cha nne sikutaka kuendelea na masomo kwani nilijijua sina akili kubwa ya kunisaidia kufikia malengo fulani. Nikatoka Iringa kuja Dar es Salaam nikaanza kuishi na washikaji zangu gheto," anasema Anko Nzalla.
"Miongoni mwa washikaji zangu mmoja alikuwa bodaboda huyo alikuwa ananipa moyo na kuona nitafanikiwa katika sanaa. Alikuwa akipata chochote tunatumia wote hadi sasa tuna bondi (ushirikiano) kubwa. Hivyo siwezi kumsahau kwani ana mchango mkubwa."
Mchekeshaji huyo anaeleza kwa nini anaitwa Anko Zalla:
"Anko ni heshima, lakini Nzalla ni jina la ukoo. Wengi wao wanajua Nzalla ni la utani, ni jina halisi."
UTANI WAKE NA HERSI
Anko Nzalla anasema ni mshikaji wa rais wa Yanga, Hersi Said ambaye anamsapoti katika kazi za sanaa na wanataniana katika mambo ya mechi za watani wa jadi ila hujikuta anapata wakati mgumu Simba kufungwa mara nyingi na wana Jangwani.
"Japokuwa Hersi ni Yanga, lakini hajabagua katika kunisapoti. Kila tukikutana ananionyesha vichekesho nilivyofanya katika simu yake. Ananishauri nizidi kupambana na kuacha alama katika kazi yangu," anasema Anko Nzalla na kuongeza:
"Ila akianza utani wa Simba na Yanga jamaa ni mnafiki sana, ila ipo siku zamu yake ya kulia itafika... tukifungwa (Simba) anaanza kucheka na kujifanya ananionea huruma wakati furaha yake ni kuona mashabiki wa Simba tunakosa raha."
AKIIGIZA NA WANASOKA
Anasema ikitokea akapata nafasi ya kuchekesha na wanasoka mastaa kutoka Yanga kama Maxi Nzengeli atampangia nafasi ile ya uchonganishi, Denis Nkane (mchangamfu), Hersi (mchonganishi), Feisal Salum 'Fei Toto (utani) na Joshua Mutale atamuweka katika uchizi.
"Hersi ana vimaneno fulani hivi vya uchonganishi Simba ikifungwa, yaani anajifanya anakuonea huruma wakati anafurahia. Nzengeli ni mpole wa muonekano, ila ni mcharuko wa kimyakimya hivyo akifanya jambo humzanii. Fei Toto muda mwingi ni mtu wa utani, Mutale ni komedi anayejichetua akili," anasema Nzalla.

USTAA BILA PESA MZIGO
Nzalla anakiri kuwa ni changamoto kupata jina kubwa bila kuwa na pesa mfukoni, kwani ni mtihani kueleweka mbele ya jamii inayokuzunguka pindi unapokuwa unahitaji msaada kutoka kwao.
"Ni kipindi kigumu kwa mastaa kujulikana halafu ukakosa pesa. Ukipanda daladala inakuwa shida. Ukihitaji msaada inakuwa shida wakati mwingine unaonekana humaanishi ama (kuonekana kama) unawapima akili (watu).
Ninachofanya najitahidi kuishi uhalisia wangu. Nina mshikaji wangu aliyeanza kunisapoti kabla sijatoka ni bodaboda, huyo ndiye ananisaidia zaidi katika suala la usafiri, hivyo nikiwa na pesa ama sina ngumu kujua," anasema Anko Nzalla.
"Katika mitandao ya kijamii ninayoitumia kama Facebook nina wafuasi milioni 2.3, Instagram milioni moja jambo linanisaidia kupata matangazo. Lakini siku ukikosa (pesa) watu wanakuwa hawaamini wanadhani kujulikana ni kumiliki pesa, ingawa faida zake ni kupata matangazo na DM zangu nyingi ni zile zinazonipongeza kwa kazi na kuniomba nifanye nao kazi."
Pamoja na hilo anasema ana hatua tofauti na mwanzo ambapo alikuwa anakaa katika maghetto ya washikaji zake, lakini kwa sasa anajitegemea mwenyewe: "Nimepanga nina uhakika wa kula na kuwasaidia ndugu zangu ninapoweza."
USHAWISHI WA STEVE MWEUSI
Mchekeshaji huyo anasema kabla ya kuanza kuigiza alikuwa anamfuatilia zaidi mchekeshaji Steve Mweusi aliyekuwa anapenda namna ya uwasilishaji wake wa kazi kwa jamii akiwa ameuvaa uhusika.
"Nakumbuka baada ya kuanza kuigiza nilimtafuta Steve. Nilidhani kwa ukubwa wa jina lake angekuwa anavimba (kichwa) ajabu ni mtu anayetamani kuona wengine wanapanda juu na kufanya vitu vikubwa. Nimefanya naye kazi mbalimbali na ananisapoti sana," anasema Nzalla.
"Wasanii wengine ambao wananisapoti ni Mr Mwanya ananishauri vitu vingi. Nilikuwa natamani kufanya kazi na mzee Senga tayari amebakia Joti kwani ni watu ambao nawapenda na wamefanya makubwa katika tasnia hii."
Mbali na hilo anaeleza namna anavyopata sapoti kubwa kutoka kwa wanasoka baadhi yao wakiwa ni Elie Mpanzu, Awesu Awesu, David Kameta 'Duchu', Abdulrazak Hamza, Ladack Chasambi na Jonathan Sowah kutoka Simba na kwa Yanga ni Djigui Diarra, Nkane, Nzengeli, Kibwana Shomari, Dickson Job na upande wa Azam FC ni Fei Toto.
"Wachezaji wapo wengi nje na hao wanaochezea timu hizo. Wananipa nguvu ya kuona kazi yangu inaonekana. Ukiachana na hao viongozi ni injinia Hersi na tajiri Mo Dewji," anasema.
KINADADA WENYE SHEPU ZAO
Anko Nzalla amekuwa akitrendi na vichekesho akiigiza na warembo wenye makalio makubwa na hilo anafafanua akisema: "Niligundua mashabiki zangu wanapenda kontenti za aina hiyo, ingawa nabuni vitu tofauti ambavyo nahakikisha nawafikia wahusika na wanafurahia kazi zangu."
Lakini anapoulizwa kama ni aina ya wanawake anaowahitaji katika maisha yake, mchekeshaji huyo anadai anachoangalia ni upendo wa kweli na siyo mwonekano wa nje.
"Napenda mwanamke anayejua kupika, mwaminifu, tunaendana katika mitazamo ya upambanaji na upendo uongee zaidi. Hakuna kitu kigumu kuangalia mwonekano wa nje ambao unaweza ukawa mwiba baadaye," anasema Anko Nzalla, mpenzi wa muziki wa Mabantu.
Mbali na uigizaji anasema anatunga stori, mwongozaji na hushauri kwa watu wanapokuwa na kazi zao aa sanaa.
"Natumia muda mwingi kufanya kazi napenda ubunifu zaidi na kujua watu wanataka kitu gani. Kwa maisha ya kawaida nadhani nipo tofauti kidogo na wengine siyo mpenzi wa magari ya kifahari, badala yake napenda kuwekeza katika biashara na ujenzi, kwani awali nilikuwa na ndoto ya kutamani kuwa daktari ikaishia njiani maana mimi na masomo ni vitu viwili tofauti, hivyo lazima niwekeze kutumia kile ninachopata katika sanaa."
Mchekeshaji huyo anasema miongoni vitu vilivyowahi kumuumiza ni Simba ilipofungwa mabao 5-1 na Yanga katika mechi iliyopigwa Novemba 5, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
"Ilikuwa mara ya kwanza kwenda uwanjani kutazama laivu mechi ya watani. Nililia machozi, ilikuwa siku mbaya sana kwangu. Nashukuru nilikuwa na washikaji ambao walielewa maumivu yangu hivyo hawakunitania, ingawa kwa sasa nimezoea na kujipa moyo itafika zamu ya mashabiki wa Yanga kulia," anasema,
Nzalla anasema ili Simba ifanye mambo makubwa inahitaji wachezaji wa viwango vya juu wenye uwezo wa kuipatia matokeo mazuri. "Namuomba tajiri Mo Dewji atuletee Fei Toto ili asaidiane na kina Sowah, na ili Simba iwe ya kwanza kunyakua taji la Afrika."

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.