Jennifer Lopez awajibu wanaokosoa mavazi yake

Mwigizaji na mwanamuziki maarufu kutoka Marekani, Jennifer Lopez (J.Lo), amewajibu baadhi ya watu wanaomshambulia mitandaoni wakidai kuwa wamechoshwa kumuona msanii huyo akivaa mavazi yanayoonesha mwili wake kupita kiasi.
Lopez, mwenye umri wa miaka 56, wakati alipokuwa kwenye onesho la kwanza la mavazi ‘Residency’ jijini Las Vegas mapema wiki hii, ameeleza kuwa kwa sasa hajali tena kuhusu maneno ya mitandaoni na wala hayamuumizi na badala yake yamekuwa yakimfurahisha sana.
“Namshukuru Mungu nimekuwa nikifanya haya kwa muda mrefu, naweza kupuuza mengi. Kwa kweli hayana maana yoyote,” alisema Lopez mbele ya mashabiki, kwa mujibu wa video ya TikTok iliyorekodiwa na mmoja wa waliohudhuria onesho hilo.
Amesema wakati mwingine huchukulia maneno hayo kama mzaha, akiongeza kuwa baadhi ya wakosoaji hutoa kauli zinazomchekesha.
“Wakati mwingine nacheka mambo ninayoyaona mtandaoni, kwa sababu wanasema vitu vya kuchekesha pia. ‘Kwa nini huwa amevaa hivyo kila wakati? Kwa nini asivae kulingana na umri wake? Kwa nini huwa yuko uchi kila wakati?’” alisema.
Nyota huyo wa filamu kama ‘Kiss of the Spider Woman’ aliibua kicheko kikubwa kwa mashabiki alipoongeza kwa utani,akieleza “Kama ungekuwa na makalio kama haya, na wewe ungekuwa uchi pia!”
Kauli za Lopez zimezua mjadala mitandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wamempongeza kwa kujiamini na kupinga dhana za kuwapima wanawake kwa misingi ya umri au mavazi, huku wengine wakiendelea kusisitiza kuwa wasanii wanapaswa kuzingatia maadili ya jamii na sio kujibu wanacho jisikia.
Hata hivyo, Lopez amesisitiza kuwa hatawahi kuacha kuwa yeye kwa sababu ya maneno ya watu, akionyesha wazi kuwa ujasiri na kujikubali ndivyo vinavyompa nguvu kuendelea.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.