Kupitia kwenye kipindi chake cha Recap, Mtangazaji El Mando amezungumzia Show za Simba day na Yanga day hasa kwa wasanii Mbosso na Zuchu.
Anasema kila mmoja alikuwa na ubora kwenye Eneo lake hasa kwenye eneo la Tukio ambapo ni Uwanjani.
Anasema ukiondoa Ile clip ya Mbosso ambayo haikufanyika eneo la Tukio basi Zuchu ndio kafanya Ubunifu mkubwa zaidi.
Anasema Mbosso amefanya vizuri kwenye Perfomance Jukwaani namna anavyoimba na Mashabiki zake ameonyesha ubora mkubwa sana.
Kwa upande wa Zuchu yeye aliwekeza zaidi kwenye Ubunifu ila kwenye Kutoa burudani Show yake ilikuwa nzuri ila haijafika level za Mbosso.