A Zeno.FM Station BONDIA RICKY HATTON AFARIKI DUNIA NYUMBANI KWAKE

BONDIA RICKY HATTON AFARIKI DUNIA NYUMBANI KWAKE

IDDY AMAN
0

 

BONDIA Richard John Hatton, maaarufu Ricky Hatton amefariki dunia leo nyumbani kwake Hyde, Tameside, Greater Manchester akiwa ana umri wa miaka 46.
Polisi wa Greater Manchester walisema hawachukulii kifo hicho kama tuhuma.
Msemaji wa Polisi alisema; “Maafisa waliitwa na mwananchi kufika Barabara ya Bowlacre, Hyde, Tameside, saa 12.45 asubuhi ya leo ambapo waliukuta mwili wa mwanamume mwenye umri wa miaka 46. Kwa sasa hakuna mazingira yoyote yanayotiliwa shaka.”
Hatton amewahi kuwa bingwa wa dunia katika uzito wa Super-Light na wakati fulani katika uzito wa Welter katika miaka yake 15 ya kucheza ngumi za kulipwa.
Ricky Hatton amefariki wakati tayari aliweka bayana mipango ya kurejea ulingoni mwezi Desemba.
Enzi zake Hatton alipigana mapambano makubwa dhidi ya mabondia wenzake nyota duniani wakiwemo Floyd Mayweather Junior na Manny Pacquiao, wakati ushindi uliomheshimisha zaidi ni dhidi ya Kostya Tszyu.
Bondia huyo aliyefahamika kwa majina ya utani ya The Hitman,
The Manchester Mexican, The Pride of Hyde na Fatton – alizaliwa Oktoba 6, mwaka 1978 huko Stockport, England.

Kama ilivyo kwa mabindia wengine nyota duniani, Hatton pia alianzia kwenye ngumi za Ridhaa na kushinda mataji kadhaa Uingereza kabla ya kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya Vijana ya Dunia mwaka 1996 (AIBA Youth World Boxing Championships).
Baada ha kutolewa kwa utata katika Nusu Fainali ya mashindano hayo ya AIBA — majaji wanne kati ya watano wakimpa ushindi Hatton, lakini kwa sheria ya utoaji pointi Hatton alipoteza pambano kutokana na Jaji wa tano kumpa pointi 16 mpinzani wake.
Jaji huyo baadaye iligundulika alipokea rushwa hivyo akakata tamaa na ngumi za Ridhaa na kuingia kwenye ngumi za kulipwa akiwa ana umri miaka 18.
Hatton alikuwa akifanya mazoezi katika Gym ya Billy “The Preacher” Graham huko Moss Side pamoja na mabondia wengine, wakiwemo Carl Thompson na Michael Gomez.
Hatton aliyekuwa akipigana Stance ya Orthodox — hadi anakutwa na umauti amepigana jumla ya mapambano 48, akishinda 45, kati ya hayo, 32 kwa Knockouts na amepoteza matatu tu.
Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default