-->

Breaking News

YANGA KUWAALIKA BANDARI FC SIKU YA MWANANCHI

 


 Klabu ya Bandari Fc ya Kenya inatajwa kualikwa na Yanga kwenye Tamasha la Wiki ya Mwananchi ambalo kilele chake itakuwa Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Tukio la Wiki ya Mwananchi litahusisha burudani na litahitimishwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ambayo itaalikwa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amekiri kumekuwa na ugumu kupata timu nje ya Afrika Mashiriki kutokana na muingiliano wa ratiba

Nchi nyingi Afrika ligi zao tayari zimeshaanza isipokuwa Afrika Mashariki ambako michuano ya CHAN inaendelea ikitarajiwa kufika tamati August 30

Bandari Fc iliyomaliza nafasi ya nane katika ligi kuu ya Kenya msimu uliopita, huenda ikapata fursa hiyo ya mualiko

Ikumbukwe pia Wiki ya Mwananchi itafanyika siku nne kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Septemba 16, hivyo mchezo dhidi ya Bandari utakuwa wa burudani zaidi na pengine kocha Romain Folz atalazimika kupumzisha silaha zake muhimu kuelekea mchezo dhidi ya Simba

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.