-->

Breaking News

TAABU IKO PALE PALE YANGA WAMALIZA ISHU YA MZIZE KIBABE

 


 Klabu ya Yanga SC iko mbioni kumbakisha mshambuliaji wake chipukizi Clement Mzize licha ya kuvutwa na ofa kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi, imefahamika

Taarifa kutoka Makao Makuu ya klabu zimedokeza uongozi umefanikiwa kumshawishi Mzize kwa kumpa mkataba mpya utakaomfanya kusalia Jangwani hadi mwaka 2028.

Awali Mzize alikuwa na mkataba wa miaka miwili, lakini kwa sasa ameongezewa mwaka mmoja zaidi, pamoja na kupewa nyongeza ya mshahara na gari jipya.

Klabu ya Esperance ya Tunisia iliripotiwa kuwasilisha ofa ya dola milioni moja kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji huyo, ambaye alifunga mabao mawili katika michuano ya CHAN. Hata hivyo, Yanga iliweka kipaumnbele cha kumshawishi ili abaki.

Mara kadhaa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, amesema sera ya klabu ni kuhakikisha kwanza nyota muhimu wanabaki, na pale tu inaposhindikana ndipo hatua ya kuwauza hufuatwa.

Yanga imeweka malengo makubwa kwa msimu ujao, ikiwemo kutetea mataji yake yote ya ndani pamoja na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya kumuuza Stephane Aziz Ki, klabu hiyo haikuwa tayari kupoteza mchezaji mwingine muhimu, hivyo kuhakikisha Mzize anasalia kuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi msimu ujao.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.