Wizkid na Jada Pollock umri ni namba tu
Kwa sasa Afrobeat inafanya vizuri duniani. Miongoni mwa wanaoutangaza vizuri muziki huo ni staa wa Nigeria, Wizkid lakini hatuwezi kuzungumzia mafanikio yake bila kumtaja Jada Pollock maarufu kama Jada P kutoka Marekani.
Kwa takriban miaka tisa Jada P amekuwa meneja wa Wizkid mwenye mafanikio mengi, kubwa zaidi amekuwa mpenzi na mama wa watoto wawili wa mkali huyo wa kibao maarufu cha Ojuelegba (2014).
Mjasiriamali huyo katika vyombo vya habari, meneja wa muziki na vipaji, alizaliwa Oktoba 20, 1983 huko Marekani na kusoma shule za St. Saviour’s na St. Olave, Uingereza na baadaye kupata shahada kutoka Chuo Kikuu cha Westminster, London, Uingereza.
Kwa kiasi kikubwa maisha yake yalikuwa ni Uingereza alipopata shahada ya Usimamizi wa Biashara kuliko nyumbani kwao Marekani alipozaliwa miaka 41 iliyopita.
Punde tu baada ya kumaliza chuo, Jada P alianzisha kampuni ya ushauri wa chapa na mitindo, Envy Lifestyle ambayo awali ilitambulika kama Jada Style na hapo ndipo safari yake ya mafanikio ilipoanzia na mengine ni historia.
Katika kampuni aliweza kufanya kazi na wachezaji wa Ligi Kuu England (EPL) akiwemo aliyekuwa mshumbuliaji wa Chelsea, Didier Drogba ambaye alishirikiana naye katika biashara yake ya boutique.
Vilevile alifanya kazi na kaka yake msanii Akon, Bu Thiam katika kampuni yake ya usimamizi chapa, Bu Vision, LLC, ambapo aliwakilisha na alisimamia baadhi ya wanamuziki wakubwa wa kimataifa kama Chris Brown, Pia Mia na wengineo.
Huyu ndio chanzo cha mafanikio ya Pia Mia katika kazi yake ya muziki alipokuwa akifanya kazi kama meneja wake wa kila siku na hadi sasa anaheshimiwa kama mmoja wa wanawake mashuhuri katika tasnia muziki Marekani.
Malkia huyo ambaye amewahi kufanya kazi na chapa ya mavazi na mitindo, Gucci Mane kama muuzaji anatajwa kama mmoja wa wajasiriamali waliofanikiwa kutokea Marekani akiwa anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola5 milioni.
Katika chapisho lake Instagram Jada P alifichua kwamba alikutana na Wizkid mwaka 2012 alipokuwa anamsimamia staa wa Pop, Marekani, Chris Brown, lakini walianza kufanya kazi pamoja kati ya mwaka 2014/15.
“Nilikuwa nikimsimamia Chris Brown wakati huo na ndipo tulikutana, tulikuwa kwenye ziara Afrika na tukaja Lagos (Nigeria) kwenye moja ya wilaya, tulikuwa na shoo huko, Wizkid alitokea kwenye shoo hiyo,” alisema Jada P.
Hata hivyo, kabla ya Jada P kuwa meneja wa msanii huyo, tayari Wizkid alikuwa na mameneja wengine wawili ambao ni Sunday Dare na Dumi Oburota, wote hawa wanatokea nchini Nigeria.
Kwa kipindi chote walichofanya kazi pamoja, Jada P amemsaidia Wizkid kusaini mikataba minono iliyomuunganisha na majina makubwa katika tasnia ya muziki duniani kama vile Drake, R Kelly, Chris Brown, Beyonce Knowles na Justin Bieber.
Mwaka mmoja tangu kuanza kufanya kazi pamoja, Wizkid aliingia kwa mara ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 kupitia wimbo wake wa One Dance (2016) alioshirikishwa na Drake, mshindi wa Grammy mara tano.
Na wimbo wa Wizkid, Essence (2020) akimshirikisha Tems ndiyo wa kwanza Nigeria kuingia chati Billboard Hot 100, Billboard Global 100, huku ukishika nafasi ya kwanza Billboard U.S Afrobeats Songs.
Billboard walimuuliza Jada P kwanini wimbo huo kutoka katika albamu ya Made in Lagos (2020) umefanya vizuri sana? Alisema kadri unavyofanya muziki watu wahusiane nao, ndivyo msukumo wa kuupenda unaongezeka.
Hadi sasa Jada P anajivunia kumpatia Wizkid tuzo ya kwanza ya Grammy mwaka 2020, huku akishinda tuzo nyingine kubwa kama BET (4), Soul Train Awards (3), Billboard Awards (3), iHeartRadio Music Awards (2) na America Music Awards (1).
Na baadaye wawili hao walizama katika mapenzi ila wakosoaji mtandaoni walimvaa mrembo huyo kwa madai ni mkubwa kiumri kwa Wizkid. Jada (41) sasa alijibu hilo kupitia Insta Story.
Alisema ni kweli ila amemzidi Wizkid miaka mitano hivi, lakini ukweli amemzidi miaka saba maana Wizkid amezaliwa Julai 16, 1990 huko Lagos, Nigeria, hivyo ana miaka 34.
Jada P alisema uhusiano ulianza msimu wa wapendanao mnamo Februari 2017 na kufikia Novemba 11, 2017 wakajaliwa mtoto wa kwanza, Zion Ayo Balogun aliyezaliwa London, Uingereza na hadi sasa wana watoto wawili.
Kwa mara nyingine tena mpenzi wa Wizkid, Jada P ametema nyongo na sasa ikiwa ni baada ya kuandamwa mtandaoni na mashabiki wanaohoji ni lini ataolewa maana uhusiano wake na msanii huyo wa Nigeria ni wa miaka mingi.
Hata baada ya Davido kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Chioma, kupitia mtandao wa X, Jada P alionyeshwa kukerwa na mashabiki waliomdhihaki kwa kuishi na Wizkid kwa miaka mingi bila ndoa.
“Ni wangapi kati yenu mnaozingatia mada hii! Wengi wenu mnaoandika hamna uzoefu, maarifa au ufahamu wa nini kinahitajika ili kuwa na furaha, ndoa yenye afya na mafanikio ambayo inadumu milele!,” Jada P aliwajibu mashabiki hao.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.