Ila Roma ni mchokozi sana
Msanii wa Hip Hop Bongo, Roma ana tabia ya uchokozi kwa wasanii mwenzake na wadau, ukisikiliza ngoma zake kwa umakini utabaini hilo. Wapo walioweza kumjibu huku wengine wakiacha balaa lipite mbali.
Katika ngoma yake, K.K.K (2014) akimshirikisha Nicolazo, Roma alionyesha kushangazwa na Lady Jaydee kumjua Songa, hiyo ni baada ya Jide kumshirikisha Songa, One The Incredible, Nikki Mbishi na Mkoloni katika wimbo wake, Joto Hasira Remix.
"Wanatugawa kimakundi watumeze ona Anakonda, family lahi wallah leo Jide anamjua Songa!" anachana Roma katika ngoma, K.K.K (Karibuni Kwenye Karamu).
Songa hakukaa kimya, katika Freestyle yake, Sio Lazima (2014) alijibu 'diss' hiyo kwa kuponda ushindi wa Roma katika Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2012 ambapo alishinda kama Msanii Bora wa Hip Hop na Wimbo Bora wa Hip Hop (Mathematics).
"Uwe na tuzo ndio uwe noma, wakati umegoma hutoi funzo kwa kila ngoma," alichana Songa katika Freestyle hiyo ambayo ni refix ya wimbo wa Nikki Mbishi ft. Godzilla na Belle 9 'Sio Lazima' kutoka katika albamu, Sauti ya Jogoo (2011).
Majibizano hayo yakaibua tetesi kuwa wasanii wapo katika bifu, hata hivyo, Songa katika wimbo wake, Beef (2014) alikanusha kuwa na ugomvi na Roma kwa kueleza ni kuwekana sawa kupishana na sio bifu, hivyo mashabiki waelewe hilo.
Roma katika wimbo wake, 2030 (2013) alimchana sana Joh Makini a.k.a Mwamba wa Kaskazini kutoka kundi la River Camp na Weusi ingawa hakuna ngoma ya Joh ambayo inaonyeshaa aliwahi kumchana Roma, hivyo ni uchokozi wake tu!.
"Hata Pacho ni Mwamba ila bado anakata viuno, Kaskazini bila Tanga ni Msondo bila Gurumo" alichana Roma kutokea Tanga, hii ilikuwa ni 'diss' ya wazi kwa Joh Makini anayetokea Arusha, hauhitaji sana kuumiza akili kuelewa.
Hata hivyo, Roma hakuanzia hapo na tunaweza kupata picha kamili ya uchokozi wa Roma kwa Joh Makini na wenzake kupitia wimbo wake, Mechi za Ugenini (2012) aliposema Hip Hop haipo tu Arusha anapotokea Joh Makini.
"Shaa... wao nimewashusha Bamaga, Hip Hop ina wigo mpana usiseme tu ipo Arachuga," anachana Roma katika wimbo huo aliyomshirikisha Jose Mtambo.
Naye Joh Makini katika wimbo wake uliotoka chini ya B'Hits, Bye Bye (2011) ft. G Nako, alitema nyongo kwa mtu aliyemletea chokochoko, "Usinitafutie sababu shika lako nitakuharibu babu, pole sana kama umekushinda utaarabu".
Diamond Platnumz ni msanii mwingine ambaye Roma amempitia sana katika ngoma zake kama K.K.K, Una Akili Wewe, Kaa Tayari na Hivi Ama Vile wa kundi lake na Stamina, Rostam.
"Huyu anaikataa laki, yule anaifuata kwa Basi, yule atamfanyia fitna ang'ae kama Almasi" Roma katika ngoma K.K.K. Je, Almasi ndiye Diamond na fitna zipo katika muziki?.
Tunapata jibu lake kupitia ngoma ya Fid Q, Sumu (2016) anaposema, "Hawaamini kwenye kuunda Diamond na Alikiba wawili, wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili".
Tukija katika ngoma yake yenye utani mwingi, Una Akili Wewe (2015) akishirikiana na Baghdad, Roma anampitia tena Diamond na mzazi mwenzie, Zari The Bosslady.
"Igundulike Tiffah ni mtoto wa Linex na Zari, Jacqueline Wolper halafu ndio alikuwa dalali" anachana Roma katika ngoma, Una Akili Wewe. Na Haikushia hapo, Roma katika ngoma yake, Kaa Tayari (2016) akiwashirikisha Jose Mtambo na Darassa akaendelea na Diamond.
"Bosi kamganda Dangote kaisahau Tip Top... Manzese!" Roma katika ngoma, Kaa Tayari, hapa Bosi anayezungumziwa ni Babu Tale ambaye ni Meneja wa kundi la Tip Top Connection lilosambaratika, na sasa yupo WCB Wasafi.
Unajua Roma anamchana sana Diamond kwa vile yeye ni timu Kiba, uthibitisho kuwa Roma ni timu Kiba anatupatia Stamina katika ngoma ya kundi lao, Hivi Ama Vile (2017).
"Eti muziki una timu haya timu Kiba mpo wapi" Stamina anamuuliza Roma katika ngoma hiyo, Roma anajibu hilo kwa kueleza,"Timu hazijengi hata Wasafi wakijenga Masaki".
"Man Hip Hop haiuzi?, ah wapi you're liar (mungo)" Roma katika ngoma yake, Mechi za Ugenini na hapo ndipo alianza kumchana na Madee ambaye kipindi cha nyuma alitoa wimbo, Hip Hop Haiuzi.
Kwa mujibu wa Roma katika ngoma, Una Akili Wewe, Madee sio Rapa mzuri na hawezi Hip Hop, na kama anaweza apewe midundo migumu, anasema; "midundo ya Tamaduni apewe Madee".
Utakumbuka midundo ya Tamaduni Muzik inayotayariwa na Maproduza kama Duke Tachez, Dean Texaz, Mujwahuki, Pallah n.k, inasifika kwa ugumu, kina Nikki Mbishi, One The Inredible, Stereo, Songa, P Mawange, ZaiiD, Ghetto Ambassador, Mansu-Li n.k ndio hasa wanaiweza na imewapatia mashabiki wengi.

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.