Taarifa Mpya kutoka Simba muda huu
Michuano ya CECAFA Kagame Cup kwa mwaka huu inatarajiwa kuanza Septemba 02 hadi Septemba 16 ambapo timu 12 zimealikwa kushiriki michuano hiyo
Klabu ya Simba ni miongoni mwa timu zilizoalikwa lakini Wekundu hao wa Msimbazi, hawatashiriki kwa msimu wa pili mfululizo
Ratiba inaelezwa kuwa ndio sababu ya Simba kugomea michuano hiyo ambayo kwa miaka ya karibuni imepoteza mvuto
Simba iko Cairo ikiendelea na pre-season na wekundu hao wa Msimbazi wanatarajiwa kurejea nchini August 28
Kikitua Tanzania, kikosi cha Simba kitaendelea na maandalizi yake kuelekea Tamasha la Simba Day litakalofanyika Septemba 10 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.