-->

Breaking News

Simba waomba mechi yao dhidi ya Yanga kusogezwa mbele

 


 Mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopangwa kupigwa Septemba 16 uko kwenye hatihati baada ya klabu ya Simba kudaiwa kuomba mchezo huo usogezwe mbele kutokana na ratiba yao ya mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa

Klabu za Yanga na Simba zote zitaanzia hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) ambapo mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Septemba 19 na 21

Simba itacheza dhidi ya Gaborone United Septemba 20 huko Botswana wakati Yanga itacheza Septemba 21 dhidi ya Wiliete huko Angola

Upande wa Yanga hakuna 'kipengele' juu ya mchezo huo kupigwa kama ulivyopangwa lakini watani zao wameomba usogezwe mbele

Hata hivyo kama utasogezwa mbele huenda usichezwe kabisa kwani ligi inapaswa kuanza wiki ya mwisho ya mwezi Septemba

Katika wiki hiyo klabu za Yanga na Simba zitakuwa na ratiba za kuhitimisha mechi za hatua ya awali ligi ya mabingwa

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.