Mechi ya ligi ya Mabingwa kati ya Gaborone United vs Simba ni September 20
Msimu huu kabla ya mikiki mikiki ya ligi kuu, itaanza kampeni ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAF CL) hatua ya awali ambapo mechi za mkondo wa kwanza zitaanza kupigwa Septemba 19
Simba itaanzia ugenini dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya Botswana, Gaborone United mchezo wa mkondo wa kwanza ukipangwa kupigwa Septemba 20
Mechi ya marudiano itapigwa wiki moja baadae katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni ratiba ambayo imekaa kimtego kwani Septemba 16 Simba inakabiliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga ambapo baada ya mchezo huo italazimika kusafiri kuelekea Botswana
Zipo taarifa kuwa TFF inaweza kufanya mabadiliko ya ratiba ya mchezo huo wa Ngao ya Jamii ili kuzipata nafasi klabu za Simba na Yanga kujiandaa na mechi zao za hatua ya awali ligi ya mabingwa
Yanga ina ahueni kidogo kwa sababu wao watacheza Septemba 21 nchini Angola

No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.