-->

Breaking News

Kuhusu Tyla Kuzimia Brazil, Ukweli Huu Hapa


 Mashabiki duniani kote wamekuwa katika mshangao kuhusiana na tukio lililomtokea nyota kutoka Afrika Kusini, Tyla la kutolewa katika klabu ya usiku akiwa amebebwa huku akiwa hajitambui ambapo wengi wao wanadai kuwa alizimia.


Kufuatia na video zilizosambaa usiku wa juzi kuamkia jana Agosti 22,2025 zilimuonesho msanii huyo aliyetambulika duniani kote kupitia wimbo wa ‘Water’ akiwa amebebwa na mlinzi wake kama mtoto huku akikimbizwa kwenye gari.

Kwa mujibu wa mitandao kama Capital XTRA na The Jasmine Brand iliripoti kuwa sababu kubwa ya msanii huyo kuzimia halikuwa tatizo la kiafya bali ukweli ni kwamba Tyla alitumia pombe kupita kiasi iliyopelekea kuzima.

Aidha kwa upande wa watu wengine walioko kwenye klabu hiyo waliweka wazi kuwa siku hiyo Tyla alitumia kiasi kikubwa cha pombe na kwa muda mrefu.

Hata hivyo baada ya video hiyo kusambaa kwa haraka msanii huyo alishare chapisho kwenye mtandao wake wa Instagram akionesha kuwa yupo sawa na halikuwa tatizo la kiafya.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.