A Zeno.FM Station Viongozi Simba Wavunja Ukimya Kuhusu Tshabalala – Yatajwa Sababu Halisi ya Kuondoka Kwake

Viongozi Simba Wavunja Ukimya Kuhusu Tshabalala – Yatajwa Sababu Halisi ya Kuondoka Kwake

 



Baada ya siku mbili za tetesi na presha kubwa mitandaoni, hatimaye viongozi wa Simba SC wamevunjia kimya kuhusu saga ya Mohamed Hussein Tshabalala kuondoka klabuni na kutua kwa mahasimu wao wa jadi – Yanga SC.

Kwa mara ya kwanza, afisa mmoja mwandamizi wa Simba (jina linahifadhiwa kwa sasa) amefunguka kuwa kuondoka kwa Tshabalala hakukuwa jambo la ghafla kama inavyodaiwa, bali ni matokeo ya mivutano ya ndani na maamuzi ya kiufundi.

“Kocha mpya hakumtaja Tshabalala kwenye mipango ya msimu ujao. Aliona kuwa mabadiliko yanahitajika katika safu ya ulinzi. Haikuwa chuki, ni maamuzi ya kiufundi,” alisema afisa huyo.

Lakini kilichoibua mjadala ni madai kuwa Tshabalala hakupewa taarifa rasmi kwa heshima anayostahili.

Inasemekana kuwa alijulishwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) siku moja kabla ya usajili wake kutangazwa Yanga – jambo lililomkera sana.

“Tulimtaka aje tuzungumze uso kwa uso. Lakini tayari alikuwa ameanza mazungumzo na upande mwingine,” chanzo hicho kiliongeza kwa masikitiko.

Mashabiki wa Simba sasa wamegawanyika zaidi. Baadhi wanalaumu uongozi kwa kushindwa kumuenzi beki aliyewatumikia kwa zaidi ya miaka saba. Wengine wanasema klabu ilifanya sahihi, kwani hakuna mchezaji aliye juu ya timu.


Kwa upande mwingine, Yanga SC wamechukua fursa hii kuonesha kuwa wako makini na wanajua kuchukua waliokataliwa – huku wengine wakisema “Simba wamelala, Yanga wanakula”
Tags :-

Post a Comment

0 Comments