Mpango wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Brentford Bryan Mbeumo, 25, umekwama baada ya klabu hiyo ya London kuongeza bei yao hadi paini milioni 70. United haitaki kulipa zaidi ya £65m. (Guardian)
Liverpool wameanza mazungumzo na Eintracht Frankfurt kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 23. (Sky Sports),
Hata hivyo, Newcastle United wanasonga mbele na jaribio lao la kumsajili Ekitike kwa matumaini ya kumpanga pamoja na mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, msimu ujao. (Telegraph - subscription required)
Aston Villa ni miongoni mwa klabu za Ligi ya Primia zinazopania kumnunua winga wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21. (Mail)
Manchester United wanavutiwa na mchezaji wa Chelsea Nicolas Jackson, 24, huku Aston Villa na AC Milan pia wakifuatilia hali ya mshambuliaji huyo wa Senegal. (Time- subcription required)
Manchester United huenda wakatafuta mkataba wa kumtafuta kiungo mbadala wa Jackson jambo ambalo linaweza kumaanisha Garnacho kuhamia Chelsea. (Telegraph - subscription required)