A Zeno.FM Station Khalid Aucho Kuachwa na Yanga, Aamua Kutafuta Timu Nyingine

Khalid Aucho Kuachwa na Yanga, Aamua Kutafuta Timu Nyingine

 Kulikoni, Khalid Aucho Kuachwa na Yanga, Aamua Kutafuta Timu Nyingine

Kiungo wa Mpira, Dokta Khalid Aucho hatokua sehemu ya kikosi cha Yanga kwa msimu ujao baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa mchezaji @justinekessytz ni kwamba Khalid Aucho amepata ofa nzuri kutoka Vietnam ambayo itampatia Mkataba wa miaka miwili ,signing fee ya takribani Bilioni moja na mshahara wa takribani Milioni 40 kwa mwezi.

Upande wa Yanga walimpatia Ofa ya Mkataba wa Mwaka mmoja ambao ungemuwezesha kupata takribani Milioni 100(Signing Fee) na mshahara unaokadiriwa Milioni 19 kwa mwezi.

Kikwazo ni kuwa Aucho aliarifiwa na Uongozi wa Yanga kuwa hatopata nafasi kubwa ya kucheza mara kwa mara katika kikosi chao kutokana na ujio wa mchezaji mpya katika eneo la kiungo!

Yanga wamechukua tahadhali hiyo kwakuwa nyota huyo amekua akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara lakini pia umri umezidi kusogea zaidi.

Kwa kifupi Aucho ameona bora nusu shari kuliko shari kamili.

Tags :-

Post a Comment

0 Comments