Tetesi za Soka Ulaya : Madrid wanamfuatilia Saliba, Utd kusajili wawili zaidi - IDDYNATION SITE

Breaking News

Tetesi za Soka Ulaya : Madrid wanamfuatilia Saliba, Utd kusajili wawili zaidi

 gReal Madrid wanamfuatilia beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 24 (L'Equipe).

Bosi wa Manchester United, Ruben Amorim, anataka kusajii wachezaji wawili zaidi katika dirisha hili la usajili (Mirror).

United pia wamepeleka ofa kwa ajili ya mshambuliaji wa Sporting Viktor Gyokeres, 27, na wanatumai wanaweza kumshawishi ajiunge nao na kuiacha Arsenal (A Bola).

Na walikataliwa nia yao ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Francesco Pio Esposito, 20, na Inter Milan mnamo Januari (Football Italia).

Mshambuliaji wa Cameroon Bryan Mbeumo, 25, amekamilisha vipimo vyake vya afya kwa Manchester United, na hivyo kutua Old Trafford kutoka Brentford (Fabrizio Romano

Manchester City wameweka bei ya pauni milioni 35 kwa kiungo wa Kiingereza James McAtee, 22, huku vilabu kama West Ham na Eintracht Frankfurt vikimtaka (Telegraph).

Real Madrid wako tayari kusubiri kumsajili beki wa Ufaransa anayechezea Liverpool Ibrahima Konate, 26, bure msimu ujao wa joto lakini wanaweza kutoa ofa ndogo katika dirisha hili la usajili (Football Insider).

Mkataba nono wa Saudi kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazil na Real Madrid Vinicius Jr, 25, umeondolewa mezani kwa sasa, lakini unaweza kurejeshwa tena mwaka 2026 (AS).

Tottenham wako tayari kutoa fedha inayohitajika kwa ajili ya beki wa Ukraine na Bournemouth Illia Zabarnyi, 22 (Caught Offside).

Nottingham Forest inaongoza katika mbio za kumsajili kiungo wa Kiingereza Jacob Ramsey, 24, kutoka Aston Villa (Football Insider).

Sunderland wamejiondoa kwenye dili la pauni milioni 17.5 la kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Armand Lauriente, 26, kutoka klabu ya Italia Sassuolo (Northern Echo).

Leeds United wanataka vita ya kumfukuzia mshambuliaji wa Hispania Mateo Joseph, 21, ianze kwa matumaini wanaweza kupata fedha nyingi kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil na Fulham Rodrigo Muniz, 24 (Sun).

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.