Arsenal wako tayari kutoa mchezaji kama sehemu ya mpango wao wa kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace, Eberechi Eze (27), na wanaonekana kuwazidi kete Tottenham Hotspur katika kumsaka mchezaji huyo wa Kiingereza. (Sun)
Brentford wanataka pauni milioni 65 kwa ajili ya mshambuliaji wao Bryan Mbeumo (25), baada ya kukataa ofa za pauni milioni 55 na milioni 62.5 kutoka Manchester United kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon. (Mirror)
Mshambuliaji wa Sporting na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres (27), yuko tayari kusubiri hadi mwisho wa dirisha la usajili ili apate dili la mkopo kwenda klabu nyingine barani Ulaya iwapo uhamisho wake kwenda Arsenal hautatimia. (Sun)
Winga wa England, Jadon Sancho (25), yuko tayari kupunguziwa mshahara ili ahame Manchester United kwenda Juventus, lakini klabu hiyo ya Serie A bado haiko tayari kukubaliana na masharti ya sasa. (Il Corriere dello Sport - via The Mail)
Nottingham Forest wanamtaka winga wa PSV Eindhoven na timu ya taifa ya Ubelgiji, Johan Bakayoko (22), kama mbadala wa Anthony Elanga (23), ambaye anaelekea kujiunga na Newcastle United. (Telegraph)
Manchester United wanatarajiwa kupata pauni milioni 8 kupitia kipengele cha mauzo ya baadaye walichokiweka walipomuuza Elanga kwenda Forest mwaka 2023. (Talksport)
Forest pia wanamfikiria Malick Fofana, mchezaji mwenza wa Bakayoko katika timu ya taifa ya Ubelgiji, ambaye ni winga wa Lyon mwenye umri wa miaka 20, na pia anahusishwa na Chelsea pamoja na Bayern Munich msimu huu wa kiangazi. (Sky Sports)
Kocha wa Aston Villa, Unai Emery, anataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres (25), na yuko tayari kutoa pauni milioni 43 kwa ajili ya Mhispania huyo. (Fichajes)
Juhudi za Arsenal kumsajili beki wa Valencia, Cristhian Mosquera (21), zimesimama baada ya klabu hiyo ya La Liga kudai zaidi ya pauni milioni 20 ili kumuachia nyota huyo wa kimataifa wa Hispania. (Mirror)
Bayern Munich wamefanya mazungumzo na wakala wa Christopher Nkunku huku wakifikiria kufanya uhamisho kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa kutoka Chelsea (27). (Bild)
Napoli wamewasilisha ofa ya pauni milioni 42 kwa ajili ya mshambuliaji wa Liverpool kutoka Uruguay, Darwin Nunez (26). (Gianluca di Marzo)
Sunderland wako karibu kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Morocco Chemsdine Talbi (20) kutoka klabu ya Club Brugge ya Ubelgiji. (Fabrizio Romano)
Atalanta wamekataa ofa ya pauni milioni 45.7 kutoka kwa klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia kwa ajili ya mshambuliaji wa Italia, Mateo Retegui (26), wakihitaji pauni milioni 51.8. (Football Italia)
Everton wanataka kumsaini kipa Mark Travers (26), ambaye aling'ara akiwa kwa mkopo Middlesbrough kutoka Bournemouth msimu uliopita. (Sky Sports)