
Newcastle wanamfanya Giorgio Scalvini kuwa kipaumbele chao katika safu ya ulinzi, Mikel Arteta amewekea Arsenal muda wa ukomo wa dili la Viktor Gyokeres na Barcelona wako tayari kumnunua Luis Diaz.
Newcastle United wamemfanya mchezaji wa kimataifa wa Italia Giorgio Scalvini kuwa kipaumbele chao katika safu ya ulinzi huku Magpies wakitumai kumsajili beki huyo wa kati wa Atalanta mwenye umri wa miaka 21 kwa takriban £30m. (Times - subscription required)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ameweka siku ya mwisho ambayo ni chini ya wiki mbili kwa klabu hiyo kufikia makubaliano ya kumnunua mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 27, na mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Slovenia Benjamin Sesko huku mchezaji wa Aston Villa Muingereza Ollie Watkins, 29, akiwa chaguo mbadala. (Mirror)
Barcelona watamfuata upya winga wa Liverpool wa Colombia Luis Diaz, 28, baada ya winga mwingine wa Uhispania Nico Williams, 22, kusaini mkataba mpya na Athletic Bilbao. (Fabrizio Romano

Kiungo wa kati wa Everton na Senegal Idrissa Gueye, 35, ambaye mkataba wake ulimalizika Jumatatu, ametia saini mkataba mpya wa mwaka mmoja akiwa na chaguo la mwaka mwingine. (Footmercato - in French)
Tottenham ni miongoni mwa klabu zinazoonyesha nia ya kumnunua beki wa kati wa Genoa Koni de Winter, 23, huku klabu yake ya Italia ikiweka thamani ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kuwa £21.5m. (Talksport)
Napoli wanafikiria kushindana na Manchester United na klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Pro League kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Fiorentina wa Italia Moise Kean, 25, ambaye kipengele chake cha kuachiliwa kwa euro 52m (£45m) kinamalizika tarehe 15 Julai. (Calciomercato - in Italian)

Burnley na Crystal Palace ni miongoni mwa vilabu vya Ligi ya Primia vinavyomtaka kiungo wa kati wa Napoli na Uswidi Jens Cajuste, 25 , ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Ipswich Town. (Sky Sports)
Crystal Palace pia wametoa ofa ya kumsajili beki wa kushoto wa Ajax, Borna Sosa, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia mwenye umri wa miaka 27 akiwa miongoni mwa chaguzi kadhaa ambazo kikosi cha Oliver Glasner kinafikiria kuimarisha kikosi. (Athletic - subscription required)
Inter Miami bado iko kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi, 38, kuhusu kuongezwa kwa mkataba wake wa sasa, ambao unamalizika mwishoni mwa 2025. (ESPN)