
Azam FC imemtambulisha rasmi kocha wa zamani wa AS Vita na
Al Hilal Omdurman ya Sudan Florent Ibenge kuwa kocha wao mpya kuelekea msimu ujao wa mashindano.
Ibenge ataiongoza Azam kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, mashindano ambayo anayajua vyema kutokana na kutwaa Taji hilo akiwa na RS Berkane.