Fadlu David Apewa Ofa kutoka Morocco
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu David, anaripotiwa kuwa katika maamuzi ya kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo kufuatia kupokea ofa ya kuvutia kutoka klabu moja inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.
Taarifa zinaeleza kuwa Fadlu anaonyesha nia ya kutafuta changamoto mpya nje ya Tanzania, ingawa mpaka sasa bado hajazungumza rasmi na uongozi wa Simba kuhusu suala hilo.
Iwapo ataondoka, itakuwa ni pigo kwa Simba ambayo imeonyesha mwelekeo mzuri chini ya uongozi wake, huku mashabiki wakingoja kwa hamu tamko rasmi kutoka kwa klabu au kocha mwenyewe.
Nini maoni yako kwa kocha Fadlu Davis juu ya hili aende au abaki?