
Arsenal imeungana na Chelsea, Liverpool na Manchester United katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 23 Hugo Ekitike. (Sport Bild - kwa Kijerumani, usajili unahitajika)
Klabu za Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen, Eintracht Frankfurt, RB Leipzig na Stuttgart nchini Ujerumani zinavutiwa na kiungo wa Manchester City na timu ya taifa England James McAtee, 22. (Times - usajili unahitajika)
Liverpool iko tayari kumtoa winga wa Scotland mwenye umri wa miaka 19 Ben Doak kama sehemu ya mpango wa kumsajili beki wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 24 Muingereza Marc Guehi. (Sun)
Mshambulliaji wa Sporting na timu y ataifa ya Uswidi Viktor Gyokeres, 27, ameiambia klabu hiyo nia yake ya kuondoka msimu huu wa kiangazi. (Record- kwa Kireno, usajili unahitajika)
Manchester United bado inamfukuzia Moise Kean wa Fiorentina lakini kipengele cha kutolewa kwa mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 25 (£44m) kinakamilika Julai 15. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
End of Iliyosomwa zaidi
Thomas Partey ataondoka Arsenal kandarasi yake itakapokamilika Jumatatu baada ya kiungo huyo wa kati wa Ghana mwenye umri wa miaka 32 kushindwa kufikia mkataba mpya na The Gunners. (Athletic -Usajili unahitajika)

Nottingham Forest inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Botafogo wa Brazil Igor Jesus, 24, kwa £10m. (Telegraph - usajili unahitajika)
Manchester United iko tayari kukubali dili iliyopunguzwa bei kumsajili Tyrell Malacia baada ya PSV Eindhoven kuamua kutogeuza mkopo wa beki huyo wa Uholanzi kuwa mkataba wa kudumu. (Mirror)
Sunderland ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia vinavyopania kumsajili beki wa Toulouse mwenye umri wa miaka 22 Charlie Cresswell, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 18 katika kandarasi yake. (Sun)


0 Comments