
UKITAKA KUWA MBAYA DAI CHAKO.
Kutokana na misimamo mikali kwa Fabrice Ngoma juu ya kudai stahiki zake uongozi wa Simbasc umeamua kusitisha mpango wa kumuongezea mkataba mpya nyota huyo DR Congo
Taarifa za ndani zinaeleza kwamba kumekuwa na utaratibu wa kucheleweshwa kwa bonasi za wachezaji kitu ambacho kikapelekea migomo ndani ya kikosi hicho kwenye michezo ya mwisho wa ligi huku Fabrice Ngoma akitajwa kama kiongozi wa alakati hizo
Ikumbukwe kua miongoni mwa sifa za wachezaji wengi kutoka Congo mara nyingi wanakuwa na misimamo mikali juu ya haki zao na awanaga mapenzi wao wanaamini kwamba wamekuja kufanya kazi na sio vinginevyo
Tofauti kabisa na wachezaji wetu wa kitanzania wao wanaweka mbele mapenzi kabla ya maslahi yao binafsi kwa ngoma ni tofauti
Rasmi sasa Simbasc wameanza mchakato wa kumtafuta mbadala wa Ngoma hili kuboresha kikosi hicho kwa msimu ujao.