A Zeno.FM Station Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Rodrygo mguu ndani mguu nje Arsenal

Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Rodrygo mguu ndani mguu nje Arsenal

IDDY AMAN
0


 Rodrygo,

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Rodrygo

Mpango wa Arsenal wa kumsajili winga wa Real Madrid, Rodrygo, 24, umekwama kutokana mchezaji huyo wa Brazil kutaka mshahara wa pauni milioni 10.2 kwa mwaka. (AS)

Mchezaji anayesakwa na Liverpool, Marc Guehi, 24, yuko tayari kumalizia mwaka wake wa mwisho wa mkataba na Crystal Palace ikiwa beki huyo wa kati hatapata ofa inayofaa kwa mustakabali wa soka lake, licha ya klabu ya Eagles kutaka kumuuza beki huyo wa England katika msimu huu wa usajili wa majira ya joto (Guardian)

Mabingwa wa Italia, Napoli, wamejiunga na Inter Milan katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Denmark wa Manchester United, Rasmus Hojlund, 22, ambaye yupo tayari kuuzwa na Ruben Amorim (Gazzetta Dello Sport)

Klabu ya Saudi Arabia, Al-Hilal, iliulizia kuhusu kiungo wa Napoli, Scott McTominay, 28, lakini klabu hiyo ya Serie A haikujadili hata mpango huo kwani haina nia ya kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland. (Football Italia)

s

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Nicolas Jackson

Chelsea wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Senegal, Nicolas Jackson, 24, huku klabu za Italia Juventus na Napoli zote zikionyesha nia ya kumtaka. (Gianluca Di Marzio)

Tamaa ya Arsenal kuimarisha safu yao ya kiungo inaweza kupelekea klabu hiyo kufanya harakati za kumsajili kiungo wa Denmark anayechezea Brentford, Christian Norgaard, 31. (Mirror)

Mlinda mlango wa Manchester United, Andre Onana, 29, anataka kubaki na kupigania nafasi yake huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon akisakwa na Monaco. (Guardian)

Bayern Munich bado wana matumaini ya kumsajili winga wa Hispania, Nico Williams, 22, kutoka Athletic Bilbao, licha ya kuwa kuna makubaliano tayari yamefikiwa kati ya mchezaji huyo na Barcelona. (Mundo Deportivo)

Marcus Rashford

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Marcus Rashford

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, 27, hajatoa matumaini ya kuhamia Barcelona licha ya klabu hiyo ya Catalans kuwa karibu kumsajili Williams. (Times)

Paris St-Germain wameanza tena mazungumzo ya kumsajili beki wa Ukraine, Illia Zabarnyi, 22, kutoka Bournemouth. (L'Equipe)

Winga wa Manchester United na Uingereza, Jadon Sancho, 25, anaipa Napoli kipaumbele kuhamia huko kuliko klabu nyingine ya Serie A, ya Juventus. (Sky Sports Italia)

Tags

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default