A Zeno.FM Station Mbosso na EP yake Mpya ni Moto wa Kuotea Mbali, Hizi ni Takwimu zake

Mbosso na EP yake Mpya ni Moto wa Kuotea Mbali, Hizi ni Takwimu zake

IDDY AMAN
0


EP ya @mbosso_, Room Number 3, imeweka historia mpya kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa mafanikio ya haraka ndani ya muda mfupi. Tangu kuachiwa kwake Juni 13, EP hiyo imepokelewa kwa kishindo, ndani ya siku 7 tu ikivuka streams milioni 15+ kwenye majukwaa yote ya kidigitali.

Takwimu Muhimu:

Streams Jumla: Milioni 15+ kwenye wiki ya kwanza.

Majukwaa yaliyotajwa: Apple Music, Boomplay, YouTube, Audiomack, Spotify.

Nyimbo zote 7 zimeingia kwenye chati za juu Tanzania na nje ya nchi.

Mafanikio ya Kimataifa:

Wimbo “Pawa” umeshika namba 1 kwenye Audiomack Oman, ukifuatiwa na Nusu Saa na Tena. Wimbo huo huo umeshika nafasi ya kwanza kwenye Boomplay Afrika, huku @mbosso_ akiwa msanii pekeee mwenye nyimbo nyingi Top 10 ya Boomplay Africa.

Mbosso ni msanii namba 1 kwenye Audiomack Tanzania, akiwa na nyimbo tatu za kufuatana kwenye nafasi za juu.

Boomplay Tanzania:

Nyimbo za tatu za #RN3 zimeshika nafasi ya 1, 2, 3 na 4 kwenye Boomplay Top Songs Tanzania, jambo la kipekee kwa msanii ambaye EP yake imeachiwa wiki hiyohiyo.

Albamu Namba 1 Tanzania:

EP hii imetambuliwa rasmi kama albamu namba 1 kwenye majukwaa yote makubwa Tanzania:

Apple Music

Boomplay

YouTube

Spotify

Audiomack

Haya mafanikio yanathibitisha kuwa Mbosso kupitia label yake mpya Khan Music, hafanyi tu muziki mzuri, bali pia amejenga msingi imara kwenye muziki wake.

EP Room Number 3 imebadilika kutoka kuwa kazi ya kisanii hadi kuwa bidhaa inayouzika na kutikisa ndani na nje ya Tanzania. Ushirikiano wake na mashabiki, ubora wa muziki, na uzito wa maudhui ni silaha yake kuu ya mafanikio.

Room Number 3 si tu EP ya burudani, bali ni mfano hai k

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default