
Klabu ya Juventus ya Serie A ina nia ya kumsajili winga wa Manchester United Jadon Sancho msimu huu wa joto, huku mabingwa wa Italia Napoli pia wakiwa miongoni mwa wanaowania saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Chelsea. (Sky Sports, )
Wasiwasi wa Liverpool katika dirisha la uhamisho hautaendelei hadi kumnunua mshambuliaji wa Newcastle United Alexander Isak, 25, huku dili la Mswidi huyo likisemekana kuwa haliko tayari. (Telegraph – Subscription Required)
Lakini mkufunzi wa Liverpool Arne Slot ana nia ya kutaka kumnunua mlinzi wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi, 24. (Talksport),
Guehi atahamia Anfield iwapo tu atakuwa na uhakika wa kuanzishwa katika kikosi cha Liverpool. (Sky Sports)

Kipa wa Manchester United na Cameroon Andre Onana anavutiwa na Monaco inayoshiriki Ligue 1, ambayo inachunguza masharti ya mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sky Sports,)
End of Iliyosomwa zaidi
Ikiwa Onana ataondoka Old Trafford, Manchester United itamgeukia kipa wa Atalanta Mtaliano Marco Carnesecchi, 24, kuchukua nafasi yake. (Gianlucadimarzio – In Itali)
Manchester City wako tayari kumruhusu Ilkay Gundogan kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto huku klabu ya Uturuki ya Galatasaray ikifikiria kumnunua kiungo huyo wa kati Mjerumani mwenye umri wa miaka 34. (Guardian)
Mabingwa wa Ligi ya Ligue 1 Paris St-Germain wamewasilisha ofa ya pili kwa mlinzi wa Bournemouth Illia Zabarnyi ambayo ni jumla ya pauni milioni 55, lakini Cherries wanamthamini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine, 22, wanayedai kuwa na thamani ya zaidi ya pauni milioni 70. (Sky Sports)

Tottenham wameiuliza Bournemouth kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa Ghana Antoine Semenyo, 25, lakini hawataendelea kumfuatilia kwa sasa. (The Athletic – Subscription Required),
Fulham wanatafuta chaguo la kumrejesha Joao Palhinha, 29, mwaka mmoja pekee baada ya kumuuza kiungo huyo wa kati wa Ureno kwa Bayern Munich kwa mkataba wa £48m. (The Mail)
Klabu mpya katika Ligi ya Premia Sunderland ndio klabu iliyopiga hatua zaidi kuliko klabu yoyote inayomsaka Vladyslav Vanat wa Dynamo Kyiv, huku klabu hiyo ya Ukraine ikidaiwa kutaka pauni milioni 21 kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Express, nje)
Baada ya msimu mmoja akiwa kwa mkopo West Ham, mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson anaweza kuhama tena msimu huu wa joto huku Brighton wakimpeana mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa PSV Eindhoven. (Football Insider, )

Beki wa Aston Villa na Ufaransa Lucas Digne, 31, ameanza mazungumzo na Atletico Madrid kuhusu kuhamia klabu hiyo ya La Liga, ambayo inaandaa dau la ufunguzi la £8m. (Football Insider,)
Monaco inaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia Al-Ittihad kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 32, ambaye anatazamia kurejea kucheza kufuatia kupigwa marufuku kutumia dawa za kusisimua misuli. (Foot Mercato – In French)