
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Tabora United, Yacouba Songne amesema amepeleka malalamiko Fifa, baada ya kutolipwa mshahara wa miezi minne na kutomaliziwa ada ya usajili. Yacouba ambaye alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Tabora msimu huu, alipata majeraha katikati ya msimu jambo lililomfanya kukosa mechi nyingi.
Akizungumza na arena, nyota huyo alisema mkataba upo ukingoni Tabora United, lakini bado hajapewa malipo yake na pia hakumaliziwa kiasi cha ada ya usajili. “Nimeipeleka Tabora United Fifa kwa kushindwa kunilipa stahiki zangu, lakini pia sehemu kubwa ya matibabu yangu nje nalipa mwenyewe badala ya timu. Ukiachana na msharaha ambao sijaupata kwa takribani miezi minne, lakini pia hata ada yangu ya usajili sijamaliziwa mpaka sasa.” alisema Yacouba