Manchester United wametoa ofa ya euro 70m (£58.9m) ili kumsajili mshambuliaji wa Brazil Raphinha, 28, kutoka Barcelona katika majira ya msimu wa joto. (Fichajes.net)
Manchester City italazimika kulipa angalau pauni milioni 70 ikiwa inataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 22, kutoka Real Madrid. (Football Insider)
Newcastle wanataka kumbakisha mshambuliaji wa Msweden Alexander Isak katika klabu hiyo lakini wanafuatilia kwa karibu wachezaji kadhaa, akiwemo mshambuliaji chipukizi wa Ipswich, Muingereza Liam Delap, 22, na Msweden wa Sporting Viktor Gyokeres, 26, kama wachezaji wanaotarajiwa kuchukua nafasi yake ikiwa Isak ataondoka huku kukiwa na ripoti ya kutakiwa na Liverpool. (Teamtalk)
Mshambulizi wa zamani wa Marekani na Chelsea Christian Pulisic, 26, yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya na klabu ya Italia AC Milan. (ESPN)
Arsenal na Chelsea zinaonekana kuwa mbele ya Liverpool katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Ufaransa Marcus Thuram, 27, ambaye anaripotiwa kuwa na kipengele cha kuuzwa kwa pauni milioni 71. (Football Insider)
Mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen, 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray, huenda akahamia Ligi kuu ya England msimu ujao, anasema mchezaji mwenzake wa Nigeria William Troost-Ekong. (Talksport)
Tottenham Hotspur ni moja ya klabu kadhaa vya ligi kuu England zinazofuatilia maendeleo ya kiungo wa kati wa Inter Miami, Mmarekani Benjamin Cremaschi, 20. (TBR Football).
AC Milan imetuma wasaka vipaji wake kumtazama mlinzi wa Burnley Maxime Esteve, 22, huku Everton na West Ham pia zikimtaka Mfaransa huyo. (Alan Nixon)
Arsenal wanafikiria kumnunua mlinzi wa kushoto wa Ajax Mholanzi Jorrel Hato, 19, licha ya kuibuka kwa Myles Lewis-Skelly msimu huu (TBR Football)