
Mshambulizi wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 kutoka Colombia Luis Diaz anatumai Barcelona itamnunua mwishoni mwa msimu huu. (Mundo Deportivo – In Spanish)
Nottingham Forest itafufua nia yao ya kumnunua Douglas Luiz wa Juventus msimu huu wa joto, baada ya kushindwa katika ombi la Januari la kumnunua kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 26. (Tuttosport – In Itali).
Everton itamfanya beki wa kati wa Genoa, 22, Mbelgiji, Koni de Winter, kuwa shabaha ya juu ikiwa beki wa Uingereza Jarrad Branthwaite, 22, ataondoka msimu huu wa joto. (TeamTalk}
Bournemouth wanatumai kubadilisha mlinda lango wa Uhispania Kepa Arrizabalaga kwa mkopo kutoka Chelsea kuwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto. (Telegraph – Subscription Required)