
Newcastle wameungana na Manchester United, Tottenham, West Ham, Chelsea na Liverpool katika mbio za kumnunua mshambuliaji wa Lille kutoka Canada Jonathan David, 25. (i Sport)
Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Everton na England Jarrad Branthwaite, 22. (Sun)
Liverpool watachuana na Arsenal kuwania saini ya mshambuliaji wa Frankfurt Mfaransa Hugo Ekitike mwenye umri wa miaka 22 wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Mirror)
Lakini Manchester United wanakimbizana na Newcastle na vilabu kadhaa vya juu vya Ulaya kumsajili Ekitike. (Football Insider)
Nottingham Forest, Arsenal na Liverpool wanavutiwa na mshambuliaji wa Udinese na Italia Lorenzo Lucca, 24, huku Manchester United na West Ham zikimfuatilia mlinzi wa klabu hiyo ya Serie A Mfaransa Oumar Solet, 25. (Messaggero Veneto)
Mlinzi wa Liverpool na Uingereza Jarell Quansah anaripotiwa kuivutia Newcastle, lakini Reds hawafikirii kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Athletic)
Besiktas, inayonolewa na mkufunzi wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, ina nia ya kumsajili winga wa Ipswich Town Jaden Philogene, 23, kwa mkopo. (Fotomac)

Manchester City wanapanga mpango wa kumnunua tena beki wa kulia wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 24, huku Liverpool pia ikimtaka beki huyo wa Uholanzi. (Team talk)
Nottingham Forest wanavutiwa na winga wa Ubelgiji Alexis Saelemaekers, 25, kwa mkopo Roma kutoka AC Milan. (Calciomercato)
Liverpool wanatarajia ofa kubwa kutoka kwa Saudi Pro League kwa mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nunez, 25. (Football Transfers)

Tottenham Hotspur wamekataa kumuuza mlinzi wa Argentina Cristian Romero, 26, baada ya Atletico Madrid kuweka wazi nia yao. (Givemesport)
Everton wanavutiwa na wachezaji wawili wa Uingereza wa Sunderland , mshambuliaji Chris Rigg, 17, na kiungo Dan Neil, 23. (Teamtalk)
Millwall na Hibernian ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia winga wa Cheltenham Jordan Thomas, 23. (Football Insider)
Tottenham wana nia ya kumrejesha mkurugenzi mkuu wa zamani Fabio Paratici, 52, katika klabu hiyo, lakini AC Milan pia inamtaka Muitaliano huyo. (Redio Rossonera)