Wanasayansi wagundua sayari nyingine 10 zenye uhai
Wataalam
wa maswala ya angani wametangaza ugunduzi wa sayari nyengine kumi
angani ambazo huenda zinaweza kusaidia uhai.Wanasayansi wa shirika
linaloshughulikia maswala ya angani NASA wanasema kuwa data mpya
iliochunguzwa kutoka kwa darubini ya Kepler inaonyesha sayari kumi zenye
miamba ambazo zipo hatua chache kutoka kwa mkusanyiko wa nyota.
Sayari
hizo ambazo zinatoshana na dunia, zote zipo nje ya jua katika
mkusanyiko huo wa nyota.Darubini hiyo ya Kepler sasa imegundua jumla ya
sayari 50 katika maeneo tofauti yenye uhai angani.
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.