Ben Pol Ataja Sababu za Ebitoke kuwa Mke wa Ndoa Baada ya Kukutana
Ben Pol amesema kuwa mara ya kwanza kumuona Ebitoke, ilikuwa ni kupitia video za msanii huyo wa vichekesho ambapo alimchukulia kama msanii wa kawaida wa komedi, kabla ya siku moja kukutana kwenye event ya wasanii ingawa anasema mwenyewe hakumtilia sana maanani na wala hakumbuki kama alikuwepo.
Baadaye, Ben Pol anaeleza kwamba alianza kushtushwa na jinsi watu walivyokuwa wakim-tag kupitia mitandao ya kijamii ujumbe wa jinsi Ebitoke alivyokuwa anampenda ambapo awali alichukulia kawaida lakini baadaye akashangaa kuona redio, runinga na waandishi wa habari wanampigia simu na kumhoji kuhusu suala hilo.
Amesema kwamba kutokana na jinsi suala hilo lilivyozidi kuwa kubwa, hatimaye aliamua kutenga muda wa kuonana naye ili wazungumze ana kwa ana
No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.