-->

Breaking News

🎤 Davido Kutumbuiza FIFA World Cup 2026 Countdown Concert Los Angeles

🎤 Davido Kutumbuiza FIFA World Cup 2026 Countdown Concert Los Angeles

📅 June 2026 | 🌍 FIFA World Cup 2026 | 🎶 Entertainment News
Davido FIFA World Cup 2026 Concert

Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria, Davido, anatarajiwa kuwa mmoja wa wasanii wakuu watakaotumbuiza katika tamasha la FIFA World Cup 2026 Countdown Concert litakalofanyika Juni 10 ndani ya Crypto.com Arena jijini Los Angeles, Marekani.

Tamasha hilo maalum limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya kuhesabu siku kuelekea kuanza rasmi kwa Kombe la Dunia 2026 ambalo litafanyika katika nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico.

🔥 Davido na Major Lazer Jukwaa Moja

Davido atapanda jukwaani sambamba na kundi maarufu la muziki la Major Lazer linaloongozwa na DJ na mtayarishaji mashuhuri duniani, Diplo.

⭐ FIFA imechagua Davido kuwa sehemu ya burudani rasmi ya kuelekea Kombe la Dunia 2026 litakaloanza Juni 11.

⚽ FIFA Yaandaa Tamasha Kubwa

Kwa mujibu wa waandaaji, tamasha hilo litaanza saa 5:00 usiku kwa saa za Los Angeles na linatarajiwa kuvuta maelfu ya mashabiki wa soka na muziki kutoka sehemu mbalimbali duniani.

FIFA pia imeeleza kuwa majina zaidi ya wasanii wa kimataifa yatatangazwa katika siku zijazo kabla ya hafla hiyo kufanyika.

🏆 Kombe la Dunia 2026 Kuanza Juni 11

Kombe la Dunia 2026 litafunguliwa rasmi Juni 11, 2026 na kwa mara ya kwanza katika historia litafanyika katika nchi tatu tofauti ambazo ni Marekani, Canada na Mexico.

Michuano hiyo itamalizika Julai 19, 2026 ambapo mchezo wa fainali utachezwa New Jersey nchini Marekani.

🌟 Shakira, BTS na Madonna Watajwa

Taarifa zinaeleza kuwa show ya fainali ya Kombe la Dunia 2026 huenda ikapambwa na mastaa wakubwa duniani akiwemo Shakira, BTS, Madonna pamoja na majina mengine makubwa kutoka tasnia ya muziki duniani.

Wasanii wengine wanaotajwa kupewa nafasi ya kutumbuiza katika matukio ya Kombe la Dunia ni pamoja na Rema, Tyla, Future na Katy Perry.


🔍 

Davido FIFA World Cup 2026, Davido Concert Los Angeles, FIFA Countdown Concert, Major Lazer, Diplo, World Cup 2026, Afrobeat News, Davido News, FIFA Entertainment, Crypto.com Arena

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.