Rick Ross Afichua Gharama za Promise Land, Bili ya Umeme Yafikia Tsh 46 Milioni kwa Mwezi
Rick Ross Afichua Gharama za Promise Land, Bili ya Umeme Yafikia Tsh 46 Milioni kwa Mwezi
0 ameendelea kuweka gumzo mitandaoni baada ya kueleza kuwa anamiliki moja ya mabwawa makubwa zaidi ya kuogelea nchini Marekani, lililopo katika makazi yake maarufu yanayojulikana kama Promise Land nje kidogo ya Atlanta.
Jumba hilo la kifahari lililopo 1 lina ukubwa wa ekari 300, huku bwawa lake likiwa na uwezo wa kubeba takribani lita 350,000 za maji.
Mbali na kuvutia kwa muonekano wake, gharama za uendeshaji wa makazi hayo zimezua mjadala baada ya taarifa mbalimbali kudai kuwa bili ya umeme kwa mwezi pekee hufikia dola 18,000 za Marekani, sawa na zaidi ya Sh46 milioni za Kitanzania.
Matumizi ya mwaka mzima yanayojumuisha umeme, huduma za bustani, mishahara ya wafanyakazi na matengenezo ya nyumba hiyo yanatajwa kufikia dola milioni moja za Marekani kwa mwaka, sawa na zaidi ya Sh2.6 bilioni.
Wachambuzi wa maisha ya mastaa wanasema utajiri haupimwi kwa kumiliki majumba makubwa pekee, bali uwezo wa kugharamia na kuyaendesha maisha hayo ya kifahari kwa muda mrefu bila matatizo ya kifedha.


No comments
Note: only a member of this blog may post a comment.