-->

Breaking News

Manchester United Yathibitisha Kuondoka kwa Højlund

Rasmus Højlund Aaga Manchester United Baada ya Kuhamia Napoli, “Ndoto Yangu Imeisha”

Rasmus Højlund ametoa ujumbe wa hisia baada ya kuthibitishwa kuondoka Manchester United na kujiunga na Napoli kwa uhamisho wa kudumu.

Nyota huyo wa Denmark amesema kuondoka Old Trafford ni wakati mgumu kwake kwani ndoto yake ya utotoni ya kucheza Manchester United imefikia mwisho.

Katika ujumbe wake wa kuaga, Højlund aliwashukuru mashabiki, wachezaji na benchi la ufundi la Manchester United kwa msaada waliompa katika kipindi chake klabuni hapo.

Amesema licha ya changamoto alizokutana nazo, kucheza kwa Manchester United ilikuwa heshima kubwa na moja ya mafanikio muhimu katika maisha yake ya soka.

Højlund alijiunga na United mwaka 2023 akitokea Atalanta, kabla ya kujiunga na Napoli kwa mkopo uliohusisha kipengele cha ununuzi wa moja kwa moja baada ya klabu hiyo kufuzu Champions League.

Sasa ataanza sura mpya ya maisha yake ya soka nchini Italia akiwa na Napoli, ambapo anatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Antonio Conte.

Endelea kufuatilia IddyNation kwa habari zote za usajili, Premier League na soka la Ulaya.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

🔔 Enable Notifications

Get latest songs and entertainment updates instantly.